Mmoja wa washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili Bi.Anna Nicholaus akikabidhiwa fulana yenye jina lake na mmoja wa Waratibu wa shindano hilo,AJ Jonathan,wakati wa utambulisho rasmi wa washiriki hao mapema jana jioni mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika kwenye ukumbi wa alliance française,jijini Dar.Aidha pia washiriki hao wapatao ishirini walipata nafasi ya kusaini mikataba yao na pia kuelezwa utaratibu mzima wa mchakato wa Bibi Bomba 2013.
Bi.Anna Nicholaus akivalishwa fulana yake ya ushiriki kutoka kwa mmoja wa waratibu wa shindano hilo lenye msisimko mkubwa,Asmah Makau.
Mshiriki mwingine wa shindano la Bibi Bomba.Bi.Tabitha Tungaraja akishukuru Mungu mara baada ya jina lake kutajwa na kuingia kwenye ushiriki wa shindano hilo,mbele ya baadhi ya waratibu wa shindano zima
Pichani wa pili kushoto ni Meneja wa Clouds TV ambao ndio warushaji wa shindano la Bibi Bomba season 2,Bwa.Lee Ndayisaba akifafanua jambo mbele ya washiriki wa shindano hilo na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana uendeshaji na mchakato mzima wa shindano hilo ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji.Shoto ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo Babuu wa Kitaa (Clouds TV),tatu shoto ni wawakilishi wa shirika la USAID,Bi.Naomi Kaspar pamoja na Dkt.May Bukuku, ambao wametoa mchango mkubwa kufanikisha maandalizi ya shindano hilo.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili 2013 wakiwa ndani ya ukumbi wa alliance française wakisiliza mchakato mzima wa utaratibu wa shindano hilo.
Shindano hilo lilianza mchakato wake wa usaili katika viwanja vya Leaders Club, ambapo Mabibi zaidi ya 60 walijitokeza aidha kati yao waliingia katika mchujo wa awali na kupatikana Mabibi 20 ambao wameendelea kupigiwa kura hadi hii leo.
Shindano la Bibi Bomba season 2 limezinduliwa rasmi hapo jana katika ukumbi wa Alliance Française, ambapo bibi 20 wanaingia rasmi katika kinyanganyiro cha kumtafuta bibi Bomba kwa mwaka 2013.
"siku zote panapokuwa na watu wengi lazima vituko, kero ama ubabe lazima vinanafasi ya kujitokeza ili kutimiza ule msemo wa kiswahili unaosema “penye wengi kuna mengi” ..tunatarajia msisimko wa aina yake katika mashindano haya kwa mwaka huu.
tofauti pia na mwaka jana ambapo shindano hili lilidumu kwa mwezi mmoja,na mwaka huu Bibi bomba itachukua takriban miezi 3.Mengi mtayapata wakati kipindi kikiwa kinaruka kuanzia saa mbili na nusu usiku",alimaliza kusema Lee wa Clouds TV ,kituo ambacho kitakuwa kikirusha shindano hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.