Timu ya waandishi wa Habari mkoa wa Mara. |
Musoma
WAKALA wa barabara (TANROADS) mkoani Mara imepiga tafu na kusaidia kupatikana kwa seti moja ya jezi,mpira pamoja na maji ya kunywa katika bonanza la michezo la Waandishi wa Habari wa mkoa huo litakalofanyika hii leo ikiwa sambamba na maazimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (Media Day).
Akizungumzia kuhusiana na maandalizi ya siku hiyo,mratibu wa bonanza hilo George Marato amesema hadi kufikia sasa maandalizi yanakwenda vizuri baada ya Tanroads mkoani Mara kusaidia kufanikisha kwa kupatikana kwa sehemu ya vifaa vitakavyofanikisha kufanyika kwa bonanza hilo.
Amesema Tanroads Mara kupitia Meneja wake wa mkoa Emanuel Koroso wameona umuhimu wa siku hiyo kwa Waandishi wa Habari kukutana pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu taaruma ya Habari na kuamua kusaidia sehemu ya maazimisho ya siku hiyo.
"Nichukue nafasi hii kumshukuru Meneja wa Tanroads mkoa wa Mara kwa kutusaidia kupatikana kwa seti ya jezi,mpira pamoja na maji ya kutosha kwa ajili ya wale wote ambao tutajumuhika nao katika bonanza letu na maazimisho mazima ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
"Tulipomfikisha ombi letu pale ofisini kwake hakuweza kusita kutusaidia katika maandalizi yetu kuhusiana na bonanza...hivyo kwa niaba ya Waandishi wa Habari mkoani Mara tunamshukuru sana Meneja wa Tanroads mkoa wa Mara kwa kile alichotoa katika kutaka kutufanikishia bonanza hili,"alisema Marato.
Alisema katika bonanza hilo kutakuwa na michezo ya kuvuta kamba,riadha,mbio za baisikeli pamoja na mpira wa miguu ambapo timu ya Waandishi wa Habari itavaana na timu ya wakusanya mapato wa TRA mkoa wa Mara.
Mratibu huyo wa bonanza la Waandishi wa Habari alidai kabla ya kufanyika kwa bonanza hilo watakutana na wadau wa soka pamoja na michezo mbalimbali ili kuona namna ya kusaidiana na kurudisha hamasa ya michezo katika Manispaa ya Musoma pamoja na mkoa wa Mara kwa ujumla.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.