Na Peter Fabian, MWANZA. 02/05/2013
MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza Bw.Wilson Mbonea Kabwe
amehamishwa Jiji la Dar es salaam
taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa naye pia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza.
Mkurugenzi Mpya wa jiji la Dar es salaam. |
Taarifa za kuhamishiwa Jiji la Dar es salaam ambalo
ni kubwa kuliko yote nchini zimekuwa zikizungumzwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa
na watumishi wa Jiji hilo lakini baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipotosha
ukweli halisi wa uhamisho wa Bw.Kabwe ambapo baadhi yao wamekuwa wakidai
amepelekwa Wizarani na wengine wakidai amehamishiwa Manispaa za Jijini Dar es
salaam.
Akizungumza na Blog hii ofisini kwake Jijini Mwanza alisema
kwamba taarifa za kwamba amehamishiwa Jiji kubwa kuliko yote nchini la Dar es
salaam niza ukweli na hata pale
alipokuwa amekwenda kuhudhulia sherehe ya maadhimisho ya Muungano na hata baada ya
kurejea kwa sasa Jijini hapa.
“Ni kweli naweza kusema kuwa nimepokea taarifa hizo
za kuhamishiwa Jiji la Dar es salaam kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo na siyo
Manispaa mojawapo kama baadhi ya watu na wanasiasa wanavyopotosha kwa umma
wakidai nimeondolewa kwa matatizo ili kupisha uchunguzi.”alisema kuwa huo ni
uzushi.
Aliongeza na kuthibitisha kwamba serikali imenihamishia
Jiji hilo kwa kuona umhimu wangu na utendaji wa majukumu yangu ili kuendana na
kasi ya ukuaji wa Jiji hilo na changamoto zinazolikabili kwa sasa katika sekta
zote za kijamii,kiuchumi na kuwezesha kupatikana maendeleo” alieleza .
Bw.Kabwe ambaye alihamishiwa Jiji la Mwanza mwaka
2006 akitokea Jiji la Mbeya na kushirikiana na viongozi wa serikali za Wilaya
ya Nyamagana na Ilemela wakati huo zikiunda Jiji la Mwanza kabla ya Augosti
mwaka kugawanyika na kuundwa Manispaa ya Ilemela sasa.
“Naondoka
Jiji la Mwanza kwa heshima, kutokana na hivi karibuni taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)kuonyesha na kulitaja Jiji la Mwanza
kupata Hati Safi ya Mapato na Matumizi ya fedha za umma kukidhi vigezo vya kupatiwa hati hiyo na kuyapita
Majiji ya Dar es salaam ,Mbeya, Arusha, Tanga na baadhi ya Manispaa na
Halmashauri za Wilaya hapa nchini”alisisitiza.
Aidha naliacha Jiji la Mwanza likiwa la Kwanza
nchini kuchukua nafasi ya kwanza (Mshindi) wa Hati ya Usafi na Mazingira kwa miaka saba mfululizo na
pamoja na frusa tele za kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali Jijini
Mwanza ambayo hii ndiyo changamoto aliyoiacha na kutakiwa mrithi wake ajaye
kuiendeleza kwa kusimamia kanuni na kuzitekeleza kikamilifu sheria za Mipango
Miji zilizopo.
Taarifa ya zinazosambazwa na kutolewa kwa kupotoshwa
na baadhi ya watu na chombo kimoja cha habari (Gazeti la kila siku nchini) Jijini
Mwanza kuwa Bw.Kabwe amihamishwa na
serikali kupisha uchunguzi wa tuhuma za mgogoro wa viwanja (Ardhi) kati ya Jiji
la Mwanza na Shirika la Hifadhi ya Mfuko wa Jamiii (NSSF) katika eneo la Bugarika Wilayani
Nyamagana kwa madai kuwa aliongoza Jiji hilo kujipatia fedha kiasi cha bilioni
1.6 ili kutoa viwanja 692 kwa NSSF lakini halikuweza kufanya hivyo.
“Ukweli na msingi wa madai hayo na Habari
zilizoandikwa na Gazeti la Mwananchi la Mei mosi ni uzushi mkubwa na zisizo na
ukweli hata chembe na iwapo kama kungekuwa na mgogoro na Shirika la NSSF nadhani
taarifa zingetolewa uongozi wa NSSF na Wizara husika na serikali ya Mkoa wa
Mwanza, suala la viwanja hivyo vinavyodaiwa ilikuwa ni makubaliano baina ya
Jiji na NSSF na liliisha malizika na hakuna mgogoro kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa
wakilipotoshwa kwa wananchi.
“Kazi ya wanasiasa ni kusema kila jambo ambalo
wanadhani ndiyo litawapatia umaarufu na mtaji wa kisiasa na njia ya kuungwa
mkono na wafuasi wa vyama vyao ili kuweza kuwachagua na kurudi madarakani Mwaka
2015 lakini watambue kuwa sisi wataalamu ni watu wa kutekeleza taratibu,kanuni
na sheria na si kuwatukuza wanasiasa na watu kwa masilahi ya yao binafsi na
vyama vyao”alisisitiza.
Sulala hili halipo kabisa ,NSSF walitaka viwanja kwenye
mradi eneo la Bugarika tulivyopima lakini ikatokea wananchi wa maeneo yale
kukubali kulipia garama ya viwanja hivyo na vikabaki viwanja vichache ambavyo
havikukidhi mahitaji ya NSSF tukawaeleza na kukubaliana na hoja yetu tukasema
kama wanahitaji basi tuwapatie eneo la kishili lililopo Katani Igoma na
siyohivyo inavyozungumzwa.
Hata hivyo mgogoro huo tayari haupo na hata Kamati
ya Bunge iliisha kutana na uongozi wa Jiji na NSSF na kusikiliza pande mbili hizo
na kumalizika kutokana na Jiji hilo kuweka bayana huku likionekana kutoa
upendeleo zaidi kwa NSSF kuwapatia maeneo ya kuwekeza ambapo ilisha toa eneo la
Mwanza Tenesi Klabu lililopo Carpili point kwa ajili ya ujenzi wa Holeli ya
hadhi ya nyota tano,eneo la kiliniki ya mbwa ambalo kwa sasa kumejengwa jengo refu la la kitega uchumi la NSSF
ikiwemo Hoteli ya JB Belamonte.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw.Baraka Konisaga
alilieleza kwamba Jiji la Dar es salaam litakuwa limepata Mkurugenzi mchapa
kazi na mtaalamu ambaye ni Mwanasheria atakaye zishughulikia changamoto
mbalimbali zinazolikabili Jiji hilo na ndiyo maana serikali imemhamishia
Mkurugenzi Kabwe kuhakikisha anashirikiana na wakurugenzi wa Manispaa na
serikali kuu kuzitafutia ufumbuzi.
“Jiji la Dar es salaam linazo changamoto nyingi na
zinazo hitaji ubunifu na utekelezaji wa sheria na Bw.Kabwe ni Mwanasheria mzuri
na mtu anayejiamini, haya madai kuwa ameondolewa Mwanza kupisha uchunguzi ni
uzushi lengo ni kumchafua lakini huwezi kuhamishwa ukapewa kituo kikubwa cha
kazi kama Jiji la Dar es salaam kama unatuhumiwa kwa madai hayo yangekuwa na
chembe ya ukweli basi angepelekwa Wizarani aidha akasimamishwa sio kuhamishiwa
Jiji kubwa kuliko yote nchin”alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Baadhi ya watu walimuelezea Bw.Kabwe kuwa ni
Mkurugenzi makini ambaye anaifahamu kazi yake na amekuwa na msimamo ambao kwa
namna moja umekuwa ni kikwazo cha baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara
wanaorahisisha mambo na tangu kuwahamishiwa Jiji la Mwanza kumekuwa na
mabadiliko makubwa katika sekta ya Uwekezaji,Miundombinu,Mipangomiji,Afya,Elimu
na Usafirishaji.
Meya wa Jiji la Mwanza Bw.Stanislaus Mabula (CCM) alisema
kwamba taarifa ya kuhamishwa kwa Mkurugenzi Kabwe anaisikia na kimsingi
hajapata taarifa rasimi ya maandishi na kama itakuwa kweli basi Jiji la Mwanza
ni la pili kwa ukubwa litasubilia Mkurugenzi atakayeteuliwa kushika nafasi hiyo
nay eye na Baraza la Madiwani litafanya kazi na yeyote atakayepewa nafasi kwa
vile Baraza na Watumishi ndiyo Jiji.
“Ni mapema kusema na kuzungumzia taarifa hiyo na
ninachotambua wakurugenzi wote wanateuliwa kutokana na sifa zao za utendaji
kazi hivyo sina mamlaka ya kuwajadili na Jiji la Mwanza halina mgogoro na NSSF
kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na wanasiasa ni kutaka kujitafutia umaarufu
nap engine wao ndiyo wamekuwa sasa wasemaji wa Jiji na si Baraza la Madiwani na
Mkurugenzi na timu yake”alisema Meya na kuongeza kuwa.
"Tutahakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatekelezeka
kwa kipindi cha miaka mitano tangu kupatiwa lidha ya kuunda serikali iliyopo
madarakani kwa kuhakikisha huduma zinapatikana na kutolewa kwa wananchi katika
sekta zote hapa Jijini pamoja na kuendelea kuboreshwa Nyanja za kiuchumi na
kupatikana kwa maendeleo na wakati huu si wa kampeni ni wakati wa kutekeleza
tuliyowaahidi wananchi."
Taarifa za ndani kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza zimeeleza kwamba uhamisho wa Bw.Kabwe ni wakawaida kwa watumishi wa
serikali na hazina kwele yoyote na watu wanaojaribu kutoa taarifa zenye lengo
ya upotoshaji kwa manufaa yao ama kujipatia umaarufu Fulani wa kisiasa na
kijamii niza makusudi na kuhamishwa kwake pia ni kutokana na kukaa muda mrefu
(miaka 8) eneo moja hatokea mara chache zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.