ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 6, 2013

BIASHARA YA KUUZA WATU SASA YAVAMIA SOKA

 NA. ALBERT G. SENGO: MWANZA
Biashara ya kusafirisha bianadamu ambayo kwa hapa nchini imekuwa ikionekana kutajwa kufanyika kwa baadhi ya wahamiaji haramu kutoka nje kupewa hifadhi na wazawa kwa njia za magendo pamoja na ile ya nchi kutumika kama njia ya wahamiaji kupitishwa kuelekea nchi za kusini mwa Afrika, sasa biashara hiyo imehamia kwa vipaji vya soka nchini Tanzania kutoroshwa kwenda nchi jirani.

Jijini Mwanza Mchezaji mahiri wa zamani wa timu za Pamba Fc na Kagera ambaye pia alikuwa kocha wa kituo cha timu ya vijana wadogo ya Alliance Academy ya jijini humo Furgance Novatus ametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na tuhuma za kuuza vijana watatu nchini Uganda kwa thamani ya Shilingi milioni 60 za kitanzania...
Bofya play sikiliza zaidi kisa hicho...

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Atanas Mdaula alisema kuwa waliuzwa kwa kiasi cha shilingi milioni 60 na wakati wakisafirishwa walibadilishiwa majina yao katika hati zao za kusafiria kwa nia ya kuficha ukweli, na hapa alikuwa akionyesha kikaratasi elekezi alichopewa na kocha wake Furgaency Novatus ili kuweza kujibu maswali yote safarini.

Calvin Richard (16) alisema kuwa hati yake ya kusafiria ilionyesha kuwa anaitwa Mohamed Hassan Said, huku Atanas Mdaula akibadilishiwa jina na kuitwa Majid Said Maneno na Abdalah Juma akibadilishiwa jina na kuitwa Abdulatif Mohamed.

Hati ya kusafiria ilionyesha kuwa anaitwa Abdulatif Mohamed badala ya Abdalah Juma 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,Mkurugenzi wa shule ya Alliance Academy James Bwire (pichani) alisema kuwa timu yake ya wachezaji chini ya miaka 15 ilialikwa kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka nchini Uganda na kufanikiwa kutwa ubingwa hivi karibuni.

Bwire alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo viongozi kadhaa wa soka nchini Uganda pamoja na Waziri wa michezo wan chi hiyo walivutiwa na uwezo wa wachezaji wake watatu ambao ni golikipa Calvin Richard(16), mshambuliaji Athanas Mdaulu(16) pamoja na mchezaji wa kiungo Abdallah Juma(15) na kuuomba uongozi kuwaruhusu kubaki nchini Uganda kwa ajili ya kuchezea katika timu za watoto za nchi hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa alikataa maombi ya waganda hao na kuwaeleza kuwa alikuwa nchini humo kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka na sio kuwauza wachezaji na kuwataka viongozi hao kama kweli wana nia hiyo kuwasiliana na wazazi wa wachezaji hao.

Lakini hatimaye Waganda hao walifanikiwa kuchukuwa mawasiliano ya kocha Fulgence Novatus aliyeingia 'kingi' na kucheza mchezo huo mchafu.

Tayari jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limemweka nguvuni kocha huyo kwa hatua za kisheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.