Miaka ya karibuni tangu kuzuka biashara ya vyuma chakavu kumekuwa na usumbufu mkubwa mitaani ya kero ya wizi wa mabomba, koki, mifuniko ya mashimo ya maji taka na hata mabango ya matangazo yaliyosimikwa kwa vyuma kung'olewa na wazisakao pesa kwa njia za mkato aka zisizo halali.
Uadimu wa vyuma hivyo uliwafanya wadau hao haramu wakusanyao vyuma chakavu kuzama hadi makaburini kudiriki hata kungoa misalaba ya chuma, watu kuona hivyo wakabuni kutengeneza misalaba ya zege, hilo halikutosha wasaka vyuma chakavu wakahamia kuing'oa hata hiyo ya zege kwenda kuiponda kuzipata nondo zilizo simikwa ndani kutia uimara....mmh!
Waungwana wakaskutiiiiii.... wakahamia misalaba ya mbao... mmh, wazee wa vyuma chakavu wakikosa vyuma wanapitia misalaba ya mbao ambayo wameigeuza dili tena kwa kwenda kuwauzia baadhi ya mafundi majeneza wasio waaminifu wanaopewa tenda kila kuchao.
Mafundi hao huipaka rangi upya kusubiri kuandika majina kwa wateja wapya.
Haija fahamika zaidi msalaba huu umefika vipi eneo hili la barabara ya Balewa jijini Mwanza eneo ambalo halina makabuli wala haliko karibu na makaburi, jeh linalosemwa na baadhi ya walinzi wa maeneo haya kwamba kuna jamaa mmoja kwenye majira ya usiku alipita akiwa amebeba lundo la vipande vikisemekana kuwa ni vya mbao ndiye kadondosha msalaba huu ni la kweli au.....!!!? Tunaelekea wapi?
Ni pale kwenye kona pembeni ya bango....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.