ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 27, 2012

KIWANDA CHA MGANGO GINNERY CHAENDELE KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI



Augustine Mgendi
BUTIAMA

Kiwanda cha Pamba cha Mgango Ginnery kilichopo katika eneo la Mgango wilaya ya  Butiama Mkoani Mara kimeendelea kujenga Mahusiano Mazuri na Wakulima kutoka mikoa ya Mara,Mwanza na Simiyu kuwaendeleza katika zao la Pamba.

Akiongea na Waandishi wa habari waliotembelea kiwandani hapo,Mkurugenzi wa kiwanda hicho Joseph Mathayo  alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza uzalishaji mwezi Julai mwaka huu ambapo msimu rasmi ulianza mwezi Juni.

Alisema Mpaka sasa Mapokeo ni Mazuri kwa wananchi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mara,Mwanza na Simiyu kitu kinachowapa nguvu ya kuendelea na uzalishaji wa Pamba,chakula cha Mifugo na Mafuta ya kupikia.

 “Kwasasa ndiyo tunaanza Msimu wetu kwa mara ya kwanza maana tunachojivunia mpaka muda huu ni kuwa mapokeo ni mazuri ya wakazi wa mikao ya Simiyu,Mara na Mwanza.”alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kulikuwa na tabu kubwa wakati wa kuanza msimu kwani Wakulima wengi hawakuwa na mtaji hivyo upatikanaji wa Pamba ukawa shida.

Bw Joseph Mathayo ambaye alijivunia ubora wa Mafuta ya kupikia yanayozaliwa na Kiwanda hicho ya nayofahamika kwa jina la Mafuta ya Radha alisema kuwa Mafuta hayo ni meupe ikilinganishwa na Mafuta mengine yaliyopo Sokoni.

 “Mafuta yetu ni Meupe sana na hii inatokana na ubora ambao tunautumia katika kuyatengeneza hivyo ni wananchi kuyajaribu kasha watupe majibu” alisema Bw Joseph Mathayo maarufu kwa jina la Rambo.

Alisema mpaka sasa kiwanda kimeajiri wafanyakazi 55 ambapo uwezo ni kuajiri wafanyakazi 70 huku vibarua wakiwa 120,Bw Mathayo aliongeza kuwa mpaka sasa zipo awamu tatu za kazi na kueleza jinsi wanavyogawa mbegu kwa wakulima na kasha kuwapa madawa.

Akiongelea changamoto zilizopo alisema ni pamoja na Miundombinu iliyopo kwasasa huku changamoto nyingine ilikuwa ni upatikanaji wa vibali wakati kwa kuanza.

Pamoja na changamoto hizo Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wa Mikoa ya Kanda ya ziwa wanaombwa kushirikiana na Kampuni hiyo ili kuendelea kuzalisha lakini kubwa zaidi ni kuendelea kutoa ajira kwa Watanzania.

  “Nadhani kikubwa ni kushirikiana ili kiwanda kiendelee kufanya kazi lakini pia kiendelee kutoa ajira kwa watanzania yaani kama tutazalisha kisha wasituunge mkono tutafunga Kampuni” alisema Mkurugenzi huyo

Kiwanda hicho cha kinamilikiwa na Mfanyabiashara maarufu Mkoani Mara Vedastus Mathayo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa msaada Mkubwa kwa Wakazi wa Mkoa wa Mara na Mikoa Jirani kwa kutoa ajira kwa vijana walio wengi . 

Source www.mwanawaafrika.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.