Mratibu wa Sensa mkoa wa Mara Bw Ramadhan Mbega |
Augustine Mgendi
MUSOMAMKOA wa Mara umekamilisha tayari umechukua hatua za haraka za kuhakikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi linafanikiwa kama lilivyopangwa katika visiwa 30 ambavyo vimo ndani ya ziwa Victoria.
Mratibu wa Sensa mkoa
wa Mara Bw Ramadhan Mbega,alisema kuwa mbali na kuyabainisha maeneo hayo pia
imetenga maeneo ya kuhesabia watu katika maeneo ya hifadhi za taifa ya Serengeti
na mapoli ya akiba yanayopakana na hifadhi hiyo.
Alisema kwa mkoa
Mara,maeneo 3335 yametengwa kwaajili ya zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi
ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu huku kila
halmashauri ikifanya maandalizi ya kufundishia mawakala watakaofanya kazi
hiyo.
Hata hivyo Bw
Mbega,amewataka wananchi wa mkoa wa Mara kuachana na dhana potofu ya baadhi ya
watu kuwa endapo watahesabiwa katika zoezi hilo wanaweza kupoteza maisha ama
kushindwa kuzaa.
Bw.Mbega aliongeza
kuwa si kweli kuwa watu wakihesabiwa watashindwa kuzaa au kupoteza maisha na
kuongeza kuwa zoezi hilo linalenga kuwezesha taifa kupata takwimu sahihi za watu
na makazi kwaajili ya kuwahudumia vema wananchi wake.
Mbali na hivyo
mratibu huyo alimpongeza mkuu wa mkoa wa Mara Bw.John Tuppa kwa kuwa mstari
mbele kuhamasisha wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.