ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 30, 2018

RC MONGELLA AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KUUGA MWILI WA MAREHEMU ISAACK GAMBA


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ameongoza mamia ya waombolezaji, wanahabari, wadau na wananchi kuagwa mwili wa marehemu Isack Muyenjwa Gamba baada ya kuwasili jijini Mwanza ukitokea jijini Dar es salam kwenye viwanja vya Ofisi za Umoja wa Klabu za Wandishi wa Habari Tanzania (UTPC) jijini Mwanza akipelekwa kijijini kwao Wilayani Bunda mkoani Mara atakako zikwa kesho.

Akitoa salamu za pole kwa wanahabari, marafiki, wananchi, jamaa wa marehemu Gamba  na viongozi wa dhehebu la Waadventist wasabato, Mongela amesema taifa na Tansinia ya wanahabari imempoteza mmoja ya watu waliokuwa mabalozi wa kuitangaza nchi yetu kimataifa na wanahabari.

“Nimimfahamu Gamba baada ya kukutanishwa naye na Mwakitwange na tangu hapo tulikuwa tukizungumza naye na kusalimiana wakati Fulani kabla ya kuondoka kwenda Idhaa ya Kiswahili ya DW lakini alikuwa mtu mcheshi na anayependa wenzake muda wote uliomkuta,”alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa UTPC, Abubakar Khassan alimwelezea marehemu Gamba kama zawadi ambayo tulipewa na mwenyezi mungu lakini ghafla ameamua kuichukua na kutuacha tukitafakari bila majibu na hata kwa kutoa neno lake la mwisho la kutuaga na kutupatia .

“Marehemu Gamba nilimfahamu wakati akifanyakazi Kampuni ya Sahara Midea Group inayomiliki Kituo cha Radio Free Afrika (RFA) na Star Televition cha jijini Mwanza kwa miaka saba ni mtu ambaye maelezo yake ni mengiu kumuelezea lakini hakuwa mtu wa kununa na kukasilika alipenda wanahabari wenzake na aliishi maisha ya kawaida hivyo tunao wajibu wa kujifunza kwa Gamba,”alisema Kassan.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba baada ya kupata taarifa kuwa marehemu Gamba atazikwa kijijini kwao Wilayani Bunda tuliona ni vyema tukawaomba ndugu watukubalie nasi tumuage kwa kuwa aliweza kuishi na kufanya kazi hapa jijini Mwanza kwa miaka isiyopungua saba katika kituo cha RFA isingependeza marafiki na wanahabari wenzake wasimuage hivyo tuliupo kubaliwa tunashukuru.

Kwa upande wake Mtangazaji wa DW Sudi Mnete  alimwelezea kwa ufupi kuwa marehemu Isack Muyenjwa Gamba alimpokea na kufanya naye Kituo cha Radio Uhuru na Radio One kabla ya yeye kutangulia nchini Ujerumani kujiunga na kufanya kazi DW hadi walipoungana na kuwa bosi wake licha ya kumpokea na kumsaidia kupata makazi ya kuishi nchini humo.

“Alikuwa hana tabia kama za Wajerumani za kutosalimiana yeye alikuwa anatabia ya kusalimia kila mtu na hata majirani huko nchini ujerumani wanatambua alama aliyowaachia marehemu Gamba ni kusalimiana nao na hata baada ya kifo chake kila mmoja alimkumbuka kwa tabia yake ya kuwasalimia na kuongea nao kwenye basi akienda kazini na alipokuwa akirudi nyumbani kwake,”alisema.

Mkurugenzi wa Radio One na ITV, Deo Rweyunga alisema kwamba katika kufanya kazi na Isack Gamba kwa muda katika Kampuni ya IPP hakuwahi kumuona marehemu Gamba akijikweza na kuwa alikuwa mtu wa watu wote na hata mkikwaruzana kwenye majukumu alikuwa akayi na kinyongo rohoni mambo yakiisha ni rafiki hivyo ni mtu wa kuigwa na kutufunza sote tunaomkumbuka kwani hakusahau mtu na alikuwa akipita Ofisi za Radio One kutusalimia alipokuwa akija likizo nchini.

Mtangazaji Paul James maarufu PJ alimwelezea Gamba kama mtu waliyeanzanaye maisha wakipanga chumba kimoja wakati wakifanya kazi Radio Free Afrika kabla ya kuhamia jijini Dar es salaam ambapo Isack alipata kuajiliwa Radio Uhuru kisha Radio One huku yeye akifanikiwa pia kwenda Radio Uhuru na Radio Clouds FM huku wakiishi pamoja na kueleza kuwa ameguswa na kupoteza rafiki aliyempenda na kuwasiliana naye muda wote.






Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.