ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 25, 2018

MAFURIKO YAUWA 7 NA WENGINE 12 HAWAJULIKANI WALIPO.

 Watu 7 wameripotiwa kufariki na wengine 12 hawajulikani walipo kufuatia mafuriko yaliotokea nchini Vietnam ambayo yamesababishwa na maporomoko ya ardhi.

Taarifa iliyotolewa na kituo cha utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa mvua zitaendelea kunyesha  katika eneo hilo, na kutoa tahadhari kwa raia waishio katika maeneo hayo.Kusini-Mashariki mwa bara la Asia kila mwaka hutokea mafuriko na maporomoko ya ardhi yanayosababisha maafa na uharibifu, ambapo watato wamefariki katika eneo la Lai Chau na wengine  wawili Ha Giang.

 Wakati hayo yakijiri Vietnam, nchini India pia mafuriko yamesababisha vifo vya watu wanne na safari za treni zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.