Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Magdalena Mtei, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Hisabati na Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Wilfred Ringo, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Airtel na DTBi Watoa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari.
·
Airtel kuanzisha mahabara ya Kompyuta kwa wanafunzi na vijana kujifunza na kuvumbua application mbalimbali.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikian na DTBi wametoa mafunzo
kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni katika matayarisho
yakufungua maabara ya kompyuta
yanayotegemea kuzinduliwa mwezi huu.
Mafunzo
hayo yametolewa na walimu 6 toka katika Kituo cha Elimu cha Galway
nchini Ireland kwa lengo la kuwapatia uwezo , mbinu na maarifa ya
technoologia ya kompyuta ili kuweza kuwafundisha
wanafunzi watakaojiunga na kutembelea maabara hiyo ujuzi
utakaowawezeshaa kutengeneza program ndogo ndogo na baadaye kuweza
kuvumbua program kubwa zenye kuleta suluhisho kwa mahitaji mbalimbali
ya biashara na jamii.
Maabara
ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza
masomo ya Tehama kuongeza ujuzi, na kutoa mwanga kwa vijana kuwa
wabunifu kwa kuzindua application mbalimbali
ambazo zitaweza kuwaingizia kipato.
Akiongea
wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar
es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
George Mulamula alisema “ kutokana
na changamoto iliyopo kwa sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa
mara ya kwanza wanapoingia katika elimu ya chuo kikuu kumefanya kuwe na
ufinyu katika ubunifu na kutumia technologia katika ujasiriamali.
Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwaya
kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri
mdogo.
Mafunzo
haya kwa walimu tunayotoa leo ni uthibitisho wa dhamira yetu katika
kuhakikisha tunakuwa na walimu bora watakaowasaidia wanafunzi kujikita
kwenye technologia na kuwa wabunifu.
Aliongeza Mulamula.
Kwa
upande wake Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “
tumejipanga kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao kwa kuanzisha
maabara hii yenye kompyuta za kujifunzia
na kuwawezesha wanafunzi kujifunza mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha
kutanua wigo wao”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.