Wachezaji kliniki ya ARS waaswa kujituma
Wachezaji wanaoshirki kliniki ya mpira wa miguu ya Airtel Rising Stars wameaswa kujituma ili kufanikisha malengo yao ya kuwa wachezaji bora na wakulipwa nchini.
Akizungumzia kuhusu siku ya pili ya mafunzo hayo, Kocha Mkuu wa Timu ya Serengeti Boys, Bakari Shime alisema kuwa mafunzo ya leo yamelenga kumiliki mpira, kuomba na kutoa pasi. Shime aliongeza kwa ku kusema ukitaka kucheza kwa mafanikio ni lazima mchezaji awe na uwezo wa kumiliki mpira na ili kufanikisha hilo ni lazima mchezaji awe na stamina nzuri.
Kliniki ya Airtel Rising Stars ambayo ilizinduliwa jana Jumatatu inaendelea mpaka Jumamosi ambapo wachezaji bora watachaguliwa kujiunga na timu ya vijana ya Serengeti Boys pamoja na Kilimanjaro Queens
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.