ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 17, 2017

MBOWE:- KUKAMATWA KWA LOWASSA NI MUENDELEZO WA HUJMA ZA JESHI LA POLISI DHIDI YA CHADEMA

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa muda na jeshi la polisi mkoa wa Geita, kwa aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Mbowe amesema kuwa kukamatwa kwa Lowassa mjini Geita siku ya Jana ni muendelezo wa hatua za jeshi hilo kuingilia shughuli halali za chama hicho.
"Huu ni muendelezo wa Jeshi la Polisi kuendelea kuwa wakala wa Chama Cha Mapinduzi, Ni muendelezo wa Jeshi la polisi kukihujumu chama hiki pindi zinapotokea chaguzi mbalimbali kuanzia za Rais, za Wabunge, Madiwani na hata viongozi wa Serikali za Mitaa na vijiji" Alisema Mbowe
KUHUSU MAJIBU YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA GEITA KWAMBA WALIFANYA HIVYO KUMPA ULINZI LOWASSA.
Mbowe akasema  " Nimesikitishwa na kauli ya kinafiki iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita kwamba eti walifanya kitendo kile kumlinda Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Hayo ni maneno ya kudhihaki Umma, kwani haiwezekani ukamlinda mttu kwa kumkamata kumzuia kufanya shughuli yake aliyokusudia kuifanya, shughulia ambayo inamuda maalum wa kutekelezwa"
"Ukamshindisha kwenye kituo cha Polisi, ukamhamisha ofisi moja hadi nyingine, ukawapiga mabomu wananchi waliokuwa wakimpokea bila kuwa na hatia yoyote ukawapiga wandishi wa habari bila kuwa na hatia yoyote wakati wakitekeleza wajibu wao, kisha huyu unayedai kumlinda ukamtaka aandike maelezo......"
"Haijawahi kutokea duniani bali hii imetokea Geita peke yake" BOFYA PLAY KUSIKILIZA
  Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa Jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alikuwa njiani akitokea mkoani Kagera, ikiwa nimuendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho katika Kanda zake kutekeleza 'Oparesheni KataFunua' inayohusisha mikutano ya ndani. Hata hivyo aliachiwa jana jioni na leo amehudhuria kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Gold Crest jijini Mwanza.

Upinzani umekuwa ukishutumu Serikali ya Rais Magufuli kwamba, ina lengo hasi kuhusu la kuua vyama vya upinzani nchini.
Mara kadhaa imekuwa ikikosoa kauli zake dhidi ya upinzani na kwamba, mwelekeo wake unalenga zaidi kuua demokrasia kinyume na mtangulizi wake Dk. Jakaya Kikwete.








Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.