ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 17, 2017

CCM MKOA WA MWANZA YAONYA MAKADA WAKE WALIOANZA KUJIPITISHA KUSAKA UONGOZI KWENYE KATA NA WILAYA NA KUANZISHA MAKUNDI


Na Peter Fabian, 
GSENGO BLOG
MWANZA.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimeanza kufatilia nyendo za baadhi ya makada wake wanaodaiwa kuanza mikakati na kupitapita kwenye Kata na Wilaya kwa lengo la kuwashawishi wanachama wenzao kuwaunga mkono katika nafasi wanazotaraji kugombea.

Hatua hiyo inafuatia kuwepo madai ya Makada na wanachama wa Chama hicho kuanza kupishana na kupigana vikumbo katika Kata za Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kushawishi wanachama kuwasaidia pindi watakapojitosa kugombea nafasi mbalimbali huku nafasi hizo zikitajwa ni Mwenyekiti wa Kata, Wilaya, Mkoa na Ujumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ngazi ya Mkoa.

Akizungumza na GSENGO BLOG jijini Mwanza, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Elias Mpanda, alieleza kuwa CCM ni Taasisi kubwa ya kisiasa ambayo imejielekeza kuhangaika na shida na kero za watu wanyonge ambao ni wananchi na serikali yake iliyopo madarakani inalo jumumu moja tu la kutekeleza Ilani ya Uchaguzi mkuu ya 2015/2020 kama ilivyoelekeza sanjali na kushughulika na maisha ya watanzania kwa kila hali ikiwemo maendeleo ya taifa zima.

Mpanda alieleza kuwa kumekuwepo taarifa za madai na tetesi kuwa wapo baadhi ya makada wanaojiandaa kugombea nafasi katika ngazi mbalimbali za Kata, Wilaya na Mkoa kuanza harakati za chinichini wakianzisha makundi yatakayowasaidia kuwanadi kwa wanachama katika uchaguzi mkuu ndani ya Chama baada ya kutolewa ratiba inayoanzia ngazi ya mashina, matawi, Kata, Wilaya na Mkoa.

“Viongozi wamekuwa wakisisitiza na kuonya kuwa Katiba ya CCM haitaruhusu makundi na utoaji rushwa kupata uongozi hivyo nirejee kwa kuwasihi wanachama na makada walioanza kujipitisha na kuunda mtandao wa makundi na hata kudaiwa kufanya vishawishi vya rushwa wakibainika hawatapitishwa hata kama watakuwa wameshinda katika nafasi walizoomba kugombea,”alisema.

Kaimu Katibu huyo alisema kwamba uchaguzi wa ndani ya Chama chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulhman Kinana na viongozi wengine wamejipanga kuwashughulikia wanachama na makada wenye taibia ya kuendekeza na kuanzisha makundi pamoja na kutumia rushwa kupata uongozi.

“Tulipokuwa na kura za maoni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Kata ya Malya Jimbo la Sumve Wilaya ya Kwimba ndani ya Chama kulitokea halufu ya rushwa uongozi wa Wilaya na Mkoa ulifuta mchakato huo na kuanza upya na Chama kimempata mgombea sahihi ambaye sasa kinamnadi kwa wananchi ili apigiwe kura za ushindi hivyo tumejipanga kwenye hili,”alisisitiza.

Mpanda alitoa onyo kwa baadhi ya wanachama na makada kuanda watu ambao hupelekea kuwanzisha makundi na wanaposhindwa kukidhi vigezo na kuteuliwa kuwa wagombea kuanzisha chuki na usaliti ndani ya Chama jambo ambalo kamwe halitavumilika na CCM imejipanga na kuwachukulia hatua kali watakaobainika.

“Viongozi wa kitaifa wamesisitiza kwamba makundi na rushwa havina nafasi katika uchaguzi wa viongozi wa ndani ya Chama kuanzia ngazi ya tawi, shina, Kata, Wilaya, Mkoa mpaka Taifa hivyo wanaojidanganya watabue mbinu zao za kuanza kuanda makundi, kutoa rushwa na kuwachafua wenzao kwa madai hawafai kugombea zinafanyiwa kazi kwa kufatiliwa na kamwe halitaachwa liendelee na hatua kali zitachukuliwa kwani litakuwa na malengo ya kukichafua Chama na Taasisi hii kubwa ya kisiasa ,”alisisitiza Mpanda.

Mpanda amewataka wanachama na makada wa Chama hicho kuwa watulivu na ikiwezekana kuwatolea taarifa za siri wale ambao wameanza mikakati na kujipitisha Kata, Wilayani kwa malengo ya kuandaa watu ili viongozi wachukue hatua ikiwemo kuwafikisha kwenye uongozi wa sekretarieti ya maadili na kamati za siasa ili kuitwa na kuojiwa ikiwemo kuonywa badala ya kuwafumbia macho waendele kuharibu utaratibu na ukiukwaji wa Katiba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.