Kampeni ya 'DEBE NA JEMBE' kikazi zaidi...kule Joha Ngasa huku Mansour Jumanne. |
NA. ALBERT SENGO: MWANZA
Watangazaji na Ma-Dj wa kituo cha redio Jembe Fm 93.7 cha jijini Mwanza, tangu siku ya Jumatatu ya tarehe 2 mwezi October mwaka huu 2016 wako katika ushindani mkali katika kupiga debe kwenye daladala za ndani na nje ya jiji la Mwanza ambapo wamegeuka kuwa kivutio cha kutosha kwa abiria wanaotumia usafiri huo pamoja na watembea kwa miguu kwenye vituo mbalimbali vya daladala na wasikilizaji, kwani ubunifu wao umegeuka kuwa burudani na siyo kazi ya kuchosha kama wengi wanavyoichulia.
"Ni kama vile waliingia darasani kujifunza mbinu za kuita wateja na jinsi ya kuvitaja vituo mbalimbali vya Mwanza, mimi nimewapenda na huwezi kuamini kama ni wao tunaowasikiliza kupitia vipindi vyao vyenye wingi ubunifu, sikudhani kama nitawaona vijana kama wao walio nadhifu wakifanya kazi hii ambayo wengi tunaidharau, kwa kweli wamenifurahisha" Alisema Mama Linda Leonard mkazi wa Mabatini jijini Mwanza ambaye alitumia moja ya daladala ambazo wapiga debe walikuwa watangazaji wa Jembe Fm.
Abiria wamesafiri na wanaendelea kusafiri bure huku wakijishindia zawadi kemkem, kupitia daladala tofauti tofauti jijini Mwanza baada ya kulipiwa nauli na redio Jembe Fm, ambapo wadau mbalimbali na makapuni nao wamehamasika katika utoaji zawadi na kuisapoti kampeni ya DEBE NA JEMBE baada ya kuelewa manufaa yake kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela naye Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi pamoja na Kitengo cha Polisi Kikosi cha Usalama barabarani wamesikika mara kadhaa wakihamasisha wananchi ndani ya kampeni hiyo hasa eneo la Utoaji elimu kwa vijana juu ya kujituma katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, biashara, kujiajiri na ujasiliamali.
Naye Mkurugenzi wa Jembe Media Group, Kampuni ambayo ndiyo wamiliki wa kituo hicho cha redio, Dr. Sebastian Ndege almaarufu Dr. Jembe amesema kuwa kampeni hiyo imeletwa maalum kwa wananchi, wasikilizaji wa Jembe Fm mkoani Mwanza kama sehemu ya utoaji elimu kwao hasa vijana kuwaimarisha na kuwafungua kifikra ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha katika suala zima la kuchapa kazi bila kubagua aina ya kazi au kuchukulia poa shughuli ndogondogo za kijasiliamali.
"DEBE NA JEMBE ni Kampeni ya kipekee ambayo imelenga katika kukumbusha na kuhamasisha uchapakazi au kusema kusema tunataka mtu awe Jembe maana yake ni kwamba lazima achape kazi" Alisema Dr. Jembe.
Alipoulizwa kwanini kampeni hiyo imewatumia vijana wake kwenye ushiriki wa nafasi ya kupiga debe na si nyingine zaidi akasema "Tumechagua nafasi ya kond (mpiga debe) ikiwa kama sehemu ya kuikumbuka nafasi ya MPIGA DEBE kwenye daladala kwa sababu ni moja ya kati ya kazi ambazo zimesahaulika au hazitambuliki kwasababu hazijarasimishwa lakini tukumbuke kwamba MPIGA DEBE awe kwenye daladala au basi, huyu naye anapata riziki kupitia kazi halali ambayo kuna wengine wanalisha na kuzisomesha familia zao"
Kisha akaongeza "Huyu ni bora sana, sana sana...... kuliko mzururaji au yule kibaka au kijana yeyote anaye bagua kazi ile hali hana chochote mfukoni" ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Moja ya zawadi zinazotolewa na Kampeni ya 'DEBE NA JEMBE'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.