ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 2, 2016

MAAFISA WATATU WA SERIKALI WATEKETEZWA KWA MOTO DODOMA.




Picha ya Mtandao.
Picha ya Mtandao. 
CHANZO/MWANANCHI:
Watu watatu wakiwamo watafiti watatu na dereva wa Kituo cha Utafiti wa udongo na maendeleo ya ardhi Seliani mkoani Arusha wameteketezwa kwa moto wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Katika tukio hilo lililotokea jana saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Iringa Mvumi, gari walilokuwa wanatumia aina ya Toyota Hilux mali ya kituo hicho, lilichomwa moto.
Kabla ya kuchomwa moto, watafiti hao mmoja kati yao mwanamke, walivamiwa na wanakijiji cha Iringa Mvumi waliwakatakata kwa mapanga na silaha za jadi kisha kuwachoma moto hadi kufa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha hilo na akasema atatoa taarifa za tukio hilo baadaye.
Taarifa za awali zilizopatikana zimesema chanzo  cha tukio hilo ni mwanamke mmoja wa kijijini hicho kupiga yowe kuashiria kwamba ameona watu ambao anahisi ni wanyonya damu (mumiani).
Taarifa hizo zilipofika kijijini, ndipo wanakijiji wakaenda kuchoma gari na kuwaua na kuwachoma moto.
Baada ya tukio hilo, Polisi walituma makachero na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika kijijini hapo na kuanza msako mkali.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Mvumi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.