Dk. Kgwangalla akiwa meza kuu na viongozi wengine katika tukio hilo leo 6 Machi katika viwanja vya Biafra. |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo 6 Machi amezindua rasmi utoaji wa viwanja kwa wanawake wa Mkoa wa Dar Es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo pia katika Mkoa wa Dar es Salaam maadhimisho hayo yakianza rasmi hiyo leo hadi hapo kilele 8 Machi katika viwanja vya Biafra.
Ambapo Dk. Kigwangalla ameelezea kuwa, maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kuweza kufanya tathimini ya mafanikio ya kuwawezesha wanawake katika Nyanja mbalimbali na changamoto wanazokabiliana nazo.
Aidha, Dk. Kigwangalla katika tukio hilo,ametoa vyeti kadhaa vya umilikaji ardhi kwa wanawake vilivyotolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB. Pia amewaagiza maafisa maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanashinda kwenye jamii na kubaini kero na changamoto hasa wanazokumbana nazo wanawake na si kukaa maofisini ilikutoa hali na motisha kwa jamii ambayo asilimia kubwa imesahulika ikiwemo kufika ama kushiriki kwenye matukio kama hayo ya maadhimisho.
Dk. Kigwangalla hakufurahishwa na kitendo cha ushiriki mdogo wa wanawake katika shughuli hiyo huku maafisa wa maendeleo ya kijamii wakiwa ndio wenye jukumu lao na hawajachukua hatua yoyote ya kufanya hivyo katika kuwafikia wananachi na hata kuwaalika katika tukio kama hilo.
D. Kigwangalla ambeye alikuwa mgeni rasmi, pia aliweza kutembelea mabandambalimbali na kupata maelezo ya mabanda hayo ambayo asilimia kubwa yalikuwa ni ya wanawake mmoja mmoja na wale wa kwenye vikundi.
Dk. Kigwangalla akihutubia kwenye mkutano huo..
Dk. Kigwangalla akitoa hati kwa moja wa wanawake hati ambazo zimetolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB).
Dk.Kigwangalla akitoa hati hizo kwa wanawake
Dk kigwangalla akipeana mikono na mmoja wanawake anayefanya shughuli za ujasiriamali
Dk Kigwangalla akiangalia moja ya bidhaa za wajasiriamali
Dk. Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa benki ya wanawake Tanzania (TWB) namna ya akaunti ya kuhifadhi maalum ya kibubu ambayo Mwanamke anahifadhiwa fedha zake katika kibubu hicho cha kisasa.
banda la wajasiriamali
Dk. Kigwangalla akisalimiana na mmoja wa vijana wa kundi la YOPA ambao walikuwa wakitoa burudani katika shughuli hizo.
Dk. Kigwangalla akiwa katika banda la benki la DCB mbao nao wapo katika tukio hilo kwa kusaidia vikundi vya akina mama pamoja na shughuli za kimaendeleo na huduma za kifedha
Moja ya mabanda ya akina mama wanaojishughulisha na ujasilimali ambao ni walemavu wakiwa katika banda lao
Dk.Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika moja ya mabanda ya akina mama wanaoshiriki kwenye wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo yameanza leo 6 Machi na kutarajiwa kufikia tamati hiyo 8 Machi.
Baadhi ya wanawake hao wakifurahia jambo latika tukio hillo.
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya bidhaa ya mjasiriamali katika tukio hilo..
Dk. Kigwangalla akisalimiana na moja ya kundi la vijana wanaojihusisha n burundani na ujasiriamali
Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliofika katika shughuli hiyo..Dk. Kigwangalla akizindua rasmi zoezi la utoaji wa hati kwa wanawake zilizotolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB). kulia ni Mkurugenzi wa benki hiyo, BI. Magreth Chacha . Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.