KAHAMA Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuchana baadhi ya mali ikiwemo vipeperushi vya wagombea ubunge, kukutwa na maandishi yenye uchochezi dhidi ya vyama vya CCM na CHADEMA.
Mkuu wa jeshi la polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika kata ya Kahama mjini na Isaka ambapo mratibu elimu kata ya Kagongwa ambaye hakutaka kutaja jina lake alikamatwa akichana na Kuchoma moto mabango ya CHADEMA.
Aidha amesema kuwa watu wengine Jumanne Christopha na Gerald Emmanuel walikamatwa mjini Kahama wakiwa wamevaa mabango mgongoni ambayo yalikuwa yameandikwa kwa ajili ya kumkashifu mgombea urais wa chama cha mapinduzi CCM John Magufuli.
Nyandahu amesema wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya kupokea maelekezo kutoka tume ya uchaguzi kwani katika vitabu vya sheria hakunasheria inayoelekeza watu wa namna hiyo wafunguliwe mashtaka kwa kuwa sheria haijatungwa na kuanza kutumika.
Hata hivyo amewataka wananchi wote katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu kuheshimu sheria za nchi kwani vitendo vyovyote venye viashiria vya uchochezi vinatafsiriwa kuwa ni kuvunja sheria za nchi zilizowekwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.