NA PETER
BABIAN, UKEREWE.
KATIBU
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amesikitishwa na
uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kushindwa kukarabati barabara maeneo
mbalimbali na kuwa katika hali mbaya yakutopitika kirahisi na kuwa kero kwa
wananchi.
Mtaturu
alisema hayo kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa kisiwa cha Irugwa na Ukara alipowahutubia
kwenye mikutano ya hadhara alipofanya ziara kujiaonea utekelezaji wa Ilani na
maandalizi ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM taifa, Abdulahaman Kinana, anayetarajia
kuanza Juni 22 mwaka huu mkoani Mwanza.
Katibu
huyo akiwa kisiwa cha Irugwa aliwaeleza wananchi kuwa, Mbunge wa Jimbo la
Ukerewe, Salvatory Machemuli (CHADEMA) hajatekeleza ipasavyo majukumu yake ya
kuwawakirisha wananchi pamoja Halmashauri ya Wilaya kuwa chini ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo mambo yote hayaendi na hali ya maendeleo imekuwa mbaya
na kurudi nyuma.
“Barabara
za Ukerewe tangu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo mwaka 2005 hadi 2010, Getruda
Mongela alisimamia na kupigania uboreshwaji wa barabara za Ukerewe na visiwa vya Irugwa na Ukara kupitia mfuko wa barabara
waliopo wameshindwa hata kuendelea kuziboresha na sasa hazipitiki kirahisi na
zingine zimeharibika vibaya na hazipitiki kabisa, hawawezi kazi lililopo ni
kuwanyima kura ili kuwatoa,”alisema.
Aidha tangu aliposhindwa na hawa wawakirishi wa Chadema ambapo alipata ubunge wa Jimbo kama aliokota pochi ya fedha ambayo imemchanganya na kushindwa kabisa kuwa mawakirishi wa wananchi wa kupigania maendeleo na haata Halmashauri iliyo chini ya Chadema nayo imeshindwa kutekeleza yale waliyoyaahidi kwa wananchi hivyo Oktoba mwaka huu muwaondoshe kwa kuwanyima kura .
Mtaturu
alisema kuwa katika barabara zilizo na hali mbaya ni ile ya Nansio- Kitale,
Nansio – Mrutunguru hadi Irangala, Nansio – Rugezi, Nansio –Nakamwa na zile za
visiwa vya Irugwa na Ukara jambo ambalo hata mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo, ameshindwa hata kusimamia za eneo la Kata yake katika kisiwa cha Ukara
hivyo hana uwezo wa kuongoza na kusimamia maendeleo ya wananchi,”alisisitiza.
Katibu
huyo alipata fursa ya kutembelea Zahanati ya kijiji cha Irugwa ambayo
inaboreshwa kwa kupanuliwa kuwa Kituo cha Afya cha Kata ya Irugwa kwa kujengwa
jengo la wodi ya wanaume na mama na mtoto ili kusaidia kupatikana huduma na
kulazwa waagonjwa kabla ya kupewa rufaa ya kupelekwa Haospitali ya Wilaya iliyo
na umbali wa zaidi ya km 90 kutoka kisiwani humo.
“Nachangia
laki tatu katika ujenzi huu, lakini tutakuja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa,
Kinana, hapa ili kujionea utekelezaji wa Ilani ambayo inaelekeza kupatikana kwa
huduma za msingi kwa wananchi ikiwemo sekta hii ya Afya na Elimu ambapo ujenzi
wa Maabara wa sekondari ya Kata ya Irugwa uko katika hatua ya kupauliwa pamoja na kukabiliwa na changamoto ya vifaa
vya ujenzi pia kuwepo kwa majengo mapya ya Kituo cha Polisi na Mahakama
kutasaidia kupunguza uharifu na wananchi wafanye shughuli zao za masendeleo kwa
amani,"alisema.
Akiwa
Kisiwa cha Ukara, Katibu Mtaturu aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuhakikisha wanatumia
fursa ya kuwachagua wawakirishi walio bora na wenye lengo la dhati la
kuwatumikia kuwaretea maendelea badala ya kuwachagua watu wanao wagawa wakati
wa kuwatumikia na wengine kutokuwa na uwezo wa kuwaretea maendeleo.
“Wananchi
acheni kuwachagua watu kwa majaribio kwani wengi wao ni wabinafisi kulingana na
sera na misimamo ya vyama vyao hivyo ni bora mkachagua viongozi wanaotokana na
CCM kwani wanazo anuani na mahali pa kufikisha kero zenu ambazo hutekelezwa kwa
kuwashirikisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yenu,”alisisitiza.
Mtaturu
aliwatupia lawama Mbunge Machemuli na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,
Joseph Mkundi, kwa kushindwa kwao kusimami na kuboresha barabara za kisiwa cha Ukara za Bwisha – Kome,
Bwisha –Nyamanga, Bwisha –Bukungu, Bwisha-Itale, Bwisha –Malelema na Bwisha
hadi Chibasi pamoja na zile za kisiwa kikubwa cha Ukerewe kilicho na Makao
makuu ya Wilayaa hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.