Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick (katikati), akipata maelezo toka kwa banda la UTT-PID juu ya Miradi wanayofanya katika mikoa mbalimbali nchini, kulia ni Uli Mtebe Afisa Mwandamizi Mahusiano na Masoko wa Taasisi ya UTT-PID. Mkuu wa Mkoa huyo alitembelea banda hilo leo Mei 2, wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall.
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) ipo kwenye kushiriki maonyesho ya Nyumba na Makazi yanayofahamika kama DAR PROPERTY 2015, yaliyoanza leo Mei 2 na kutarajiwa kumalizika Mei 5, mwaka huu ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall uliopo Upanga, Jijini Dar es Salaam.
Katika maonyesho hayo, UTT-PID, inashiriki ikiwemo kutoa elimu mbalimbali na maelezo juu ya utendaji wa kazi za taasisi pamoja na huduma kwa watu mbalimbali wanaotembelea kwenye banda lao hilo ndani ya Diamond Jubilee V.I.P Hall.
Aidha, mapema leo Mei 2, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alipata wasaha pia wa kutembelea banda hilo la UTT-PID na kupata maelekezo kadhaa ya namna ya utendaji wa kazi wa taasisi hiyo hapa nchini.
KAZI ZA UTT-PID
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Dar Property 2015
Ni maonesho ya siku nne kuanzia Mei 2 hadi 5, ambayo wadau mbalimbali kutoka Mashirika binafsi na Taasisi za Umma zinazojihusiha na uwekezaji katika Majumba, Ardhi na Makazi wanashiriki. DAR PROPERTY, ambayo kwa mwaka huu ni ya msimu wa pili yakifanyika na kushirikisha wadau hao mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa Meck Sadik, akiuliza swali linalohusiana na mradi wa viwanja wa Lindi ambapo Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alimfafanulia kuhusu mradi kufunguliwa na sasa upanuzi na uchongaji wa barabara unaendelea hii inajumuisha na uandaaji wa Hati Miliki zaidi ya 2,500 kwa wanunuzi wa viwanja awamu ya kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick (katikati), akipata maelezo toka kwa banda la Taasisi ya UTT-PID juu ya Miradi wanayofanya katika mikoa mbalimbali nchini, kulia ni Uli Mtebe Afisa Mwandamizi Mahusiano na Masoko wa UTT-PID. Mkuu wa Mkoa huyo alitembelea banda hilo leo Mei 2, wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall.
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka wa Taasisi ya UTT-PID, akimuhudumia mmoja wa wateja waliotembelea banda la UTT-pid ndani ya maonesho ya Dar Property 2015, yanayoendelea katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall.
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka akimuhudumia moja ya wateja (Hayupo pichani) aliyetembelea banda la UTT-pid.
Moja ya mradi uliofanikisha na UTT-PID wa jengo la kisasa la Ushirika Bulding lililopo, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.