ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 15, 2013

MKAPA AKUSANYA SHILINGI MILIONI 400 KUCHANGIA UJENZI WA MAKTABA NA MAABARA CHUO KIKUU BUGANDO (CUHAS)

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akipata maelezo kuhusu ujenzi unaoendelea wa jengo la maabara na maktaba ya chuo kikuu cha Sayansi na Tiba za Afya cha Bugando (CUHAS) kulia ni Prof. William Mahalu,  Mhasham Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Geita huku anaye sikilizwa ni aliyewahi kuwa Waziri katika Utawala wa Rais Mkapa Mhe. Pius Ng'wandu

Hivi ndivyo litakavyokuwa jengo la maabara na maktaba la Chuo kikuu cha CUHAS ambalo litafahamika kwa jina la Mwalimu Nyerere ikiwa ni kumuenzi Hayati baba wa Taifa.Julius Kambarage Nyerere. 

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa akitoa hotuba iliyowavutia wachangiaji wakipiga makofi kwa kumwita 'Mzee wa ukweli na uwazi' ambapo alihamasisha wadau na waalikwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 400. 

Makamu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba za Afya cha Bugando (CUHAS) Prof. Jacob Mtabaji akitoa taarifa ya chuo na ujenzi wa Jengo la maabara, kulia kwake ni Mhasham Askofu Tarcius Ngalalekumtwa, Rais mstaafu Ben Mkapa na Mhasham Askofu Agustino Shayo wa Jimbo Katoliki Zanzibar.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Steven Wasira, Mbunge wa Magu Festus Limbu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga na Mbunge (MNEC) wa Sengerema William Ngereja.

Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi milioni 2 mbele ya mwendesha harambee Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kutoka kulia ni Six Mwiheche Kisuruli ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Six Solution, na katikati ni Injinia Chacha ambaye ni Mkandarasi wa Majengo ya Hosteli ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba  (CUHAS)

Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Charles Kitwanga 'Mawe Matatu ' (wa pili kutoka kushoto) na wa kwanza kulia ni Pius Ng'wandu aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tatu. 

Kushoto ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Madaraka Nyerere akiwa na baadhi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki ambao ni wajumbe wa Baraza kuu la maaskofu wa kanisa katoliki nchini.

Sehemu ya Madaktari wa Hospitali ya Rufaa Bugando nao walishiriki kuchangia harambee ya ujenzi. 

Director wa Isamilo Lodge ambaye pia ni MNEC wa Busega Raphael Chegeni (kulia) akiwa na mwakilishi wa Benki ya CRDB (katikati) na kushoto ni DC Angelina Mabula wa Butiama. 

Kutoka kushoto ni Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Director wa Gold Crest Hotel (MNEC wa Arumeru) Mathius Manga na Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Mesharck Bandawe.

Wadau walioalikwa  kuchangia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.