NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Moja kati ya ahadi kati ya zilizo orodheshwa ndani ya ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM ni kujenga meli kubwa katika ziwa Victoria ili kuboresha huduma ya usafiri katika ziwa hilo, ahadi iliyotolewa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wakati akiomba kura kwa wananchi Kanda ya Ziwa Victoria.
Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawsiliano ATASHTA NDITIYE amesema serikali tayari imekwishatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa meli hiyo na kushauri uongozi wa bandari kuokoa gharama za ujenzi kwa kutumia wakandarasi wa ndani katika ujenzi wa meli hiyo nakuitaka mamlaka ya mandari kutumia wandarasi wandani nakutolea mfano NDITE Hivi karibuni kampuni ya kizalendo ya SONGORO MARINE imekamilisha ujenzi wa kivuko kikubwa katika ziwa Victoria chenye uwezo wa kubeba tani 250 za mizigo, abiria 1000, pamoja na magari 36 alisema NDITIE.
Aidha waziri NDITIE amepata fursa ya kukagua muendelezo wa usafirishaji wa mizigo kutoka Tanzania hadi Uganda kupitia bandari ya Mwanza ambayo ilisitishwa kwa zaidi ya miaka kumi.Jitihada hizi za kuboresha usafiri katika ziwa Victoria, sambamba na kufufua bandari ya MWANZA ni chachu katika ukuaji wa uchumi.
Mkuu wa mkoa JOHN MONGELLA,amepokea shehena ya pili ya mabehewa 18 kwa niaba ya serikali tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini uganda yakiwa katika bandari ya mwanza kusini ambayo yatasafirishwa kwa kutumia meli ya mv umoja kutoka mwanza hadi port belly nchini uganda,aidha MONGELA,amesema kuimarika kwa bandari hii ni mwanzo mzuri na kuchochea uchumi kwa mkoa wa mwanza.
Kwa upande wake MAHAMUD MABUYU,ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji wa Shirika la chakula duniani (WFP) Tanzania, amesema usafirishaji kwa kutumia reli na meli umesaidia katika kupunguza gharama muda na usalama mizigo kutoka bandari ya DAR ESALAAM kwa asimia 40 alisema MAHAMUD kwa kusafirisha shehena hiyo kubwa ya chakula na mafuta.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.