ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 4, 2018

MONGELLA AWAONESHA NJIA WASHIRIKI MISS MWANZA 2018 AWAASA KUFANYA HAYAGSENGOtV
Washiriki 14 wa kinyang'anyiro cha kumsaka mnyange wa Miss Mwanza 2018 wametambulishwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.

Mbele ya Kamati ya Maandalizi ya shindano hilo sanjari na waandishi wa habari waliojitokeza katika ukumbi wa mikutano ndani ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mongella amesema kuwa imekuwa ni jadi kuona baada ya mashindano kufanyika, huku wakiwa na mipango yao mbalimbali yenye tija, washiriki hao hupotea licha ya kutoa ahadi mbalimbali zenye taswira ya tija kwa jamii iwapo kama zingefanyiwa kazi.

"Sasa hivi mtatuambia oooh nataka kuwa na shule ya watoto waishio mazingira magumu, mwingine anataka asaidie hiki na kile..... Nawashauri hebu ishini ndani ya ndoto zenu ili baada ya mashindano mlete mabadiliko katika jamii, kwani mimi ninaamini ndoto zenu ni sehemu ya hatua katika kusaidia jamii yetu kwenye afya, harakati za akinamama, utalii, mazingira, uchumi nakadhalika" Alisema Mongella.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.