ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 3, 2018

ASLAY & NANDY KUIPAMBA MISS MWANZA IJUMAA HII - JOKATE & HAMISA MOBETO SEHEMU YA MAJAJI USIKU HUO.

Siyo siri tena mwanadada mwanamuziki mkali anayetamba hivi sasa kwa kazi zake nzuri Nandy tayari keshaingia kwenye ratiba ya kutoa burudani usiku wa kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo wa kuvalishwa taji la Miss Mwanza 2018.

Akizungumza na GSengoTv Mkurugenzi wa Mepal Management, Ms Pamela B. Irengo  amefunguka sababu za kumteuwa Nandy kuburudisha usiku huo "Ukizungumzia wakali wanaogusa na kuburudisha kwa sasa nchini, Nandy hakosekani" Kisha akaongeza "Analimudu vyema jukwaa, ana kazi nyingi nzuri na nyingi zimekuwa kwenye play list zao iwe nyumbani kwenye Tv au hata kwenye simu zao"

Pamela ameongeza kuwa mbali na Nandy mkali mwingine anayetikisa kwa sasa kwa kazi zake kusikika kila kona huku zikipendeka si kwa vijana tu bali pia wazee hata watoto, Aslay Sihaka naye amekwisha saini mkataba wa kutumbuiza usiku huo unaotajwa kuwa utakuwa na mvuto wenye utofauti sana.

"Natamba, Nyakunyaku, Muhudumu, Nibebe, Angekuona na Likizo zote ziko kwenye list ya zile atakazo tumbuiza kwenye jukwaa la ijumaa hii ya tarehe 6 mwezi July 2018 pale Rock City Mall. Ninayofuraha kusema kuwa kila idara imekamilika kuanzia zawadi kwa mshindi amabayo itatolewa pale pale hadharani, mchoro wa jinsi jukwaa litakavyo wekwa, sound system, ma dj pamoja na ma-Mc wa shughuli" alisisitiza Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa.

MOBETO NA JOKATE WAJUMUISHWA SEHEMU YA MAJAJI

Tutakuwa na majaji watano na miongoni mwao yumo kipenzi cha wengi Hamisa Mobetto na mrembo mwingine Jokate Mogelo ambao wanasadikika kuwa na macho ya umakini katika machaguzi ya vitu vizuri vyenye tija na maslahi kwa jamii.

Hamisa Mobetto
Jokete Mogelo
Tayari warembo 14 wako kambini kumalizia hatua zao za mwisho ambapo kwa sasa licha ya kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya usafi maeneo ya sugu ya jiji pia wamepata fursa ya kupigwa darasa kwa kutembelea vituo mbalimbali vya shughuli za kijamii, ikiwa ni pamoja na sekta za afya, maji na uhifadhi wa ziwa Victoria, viwanda, biashara na utalii ili kuwakomaza katika uelewa.

Miss Mwanza 2018 inatarajiwa kushika kasi Ijumaa hii ya tarehe 06/July/2018 katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza, ambapo kiingilio kimetajwa kuwa ni shilingi 10,000/= kawaida na shilingi 50,000/= VIP.
Jumatano hii kupitia kipindi cha 'Tuongee asubuhi ndani ya Star Tv' Mkurugenzi wa Mepal Management Pamela Irengo atahusika LIVE akishiriki mada 'Sanaa na Maendeleo ya Jamii'.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.