WAKULIMA KUPIGWA MSASA JUU YA UVUNAJI PAMBA.
Na Albert G. Sengo,Igunga
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo
amesema kuwa halmashauri yake kushirikiana na bodi ya Pamba nchini (TCB) mnamo
mwezi Machi watatoa semina elekezi ya uvunaji wa zao la Pamba ili kupata
stahiki katika ubora.
Mwaipopo ametanabaisha hayo mbele ya
wandishi wa habari waliofanya ziara wilayani mwake kujioneo yanayojiri.
“Kumekuwa na changamoto kubwa sana nyakati
za mavuno, kwa wakulima wa wilaya yangu kuchuma Pamba pamoja na mashina yake,
kitendo ambacho hakikubaliki kwani huondoa sifa ya ubora wa zao hilo katika
soko la dunia”
Ameongeza kuwa kupitia kampeni ya
kuhamasisha kilimo cha Pamba waliyoifanya na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey
Wandry imeweza kuongeza idadi ya wakulima wa zao hilo wanaotoka ndani na nje ya
wilaya, kiasi kwamba hata wananchi wa mikoa ya mbali nao wamemiminika kukodisha
mashamba na kufanya kilimo cha ‘Dhahabu nyeupe’.
“Sisi Igunga bado tuna ardhi kubwa
sana wananchi wetu wanalima hapa lakini bado tunawakaribisha wananchi kutoka
maeneo mengine, ninazo taarifa kuna wakulima hapa wametoka mpaka Dar es salaam
na maeneo mengine wao wamekuja kwakuwa wameiona fursa na kuichangamkia”
“Kwa miaka miwili hii kumekuwa na
mwanga mkubwa wa mafanikio na kuona wapi tunaelekea, mfano Mwaka jana tulipata kilogramu
milioni kumi la laki saba na mwaka mmoja kabla yaani mwaka juzi tulipata
kilogramu milioni 11 hiyo ni kwasababu mwaka jana kumekuwa na hali ya ukame
unao shindana mwaka hadi mwaka, sasa kwa
hali ilivyo sasa nikimaanisha mvua za kutosha, hamasa ya wakulima wengi
kujitokeza naiona Igunga ikipaa na kuishangaza nchi katika mavuno” Aliongeza
Mwaipopo.
Kwa mujibu wa Mwaipopo mpaka sasa
wilayani Igunga kuna kata 17 na vijiji 54 vinalima zao la Pamba.
Kwa upande wake mkaguzi mwandamizi wa
zao la Pamba wilayani hapa George Kihimbi amesema kuwa uhamasishaji mkubwa
uliofanywa kwa msimu wa kilimo 2017-2018, wamedhamiria kulima jumla ya hekari
110,000.
Katika hatua nyingine licha ya
kuipongeza Serikali kwa kuwapatia mbegu na madawa kwa wakati pia ameiomba Serikali/Bodi
ya Pamba, kupitia maafisa wake na mawakala kurejea tena kwenye maeneo hayo na
kuwaongezea dawa kwani daadhi yao walikiuka masharti na kulazimika kuzigawa na
kuzielekeza dawa za awali kwenye mahindi ili kuyanusuru na wadudu waharibifu
waliolivamia zao hilo.
“Mwaka
huu tunategemea kuzalisha Tani laki 6 tofauti na Mwaka jana ambapo zilipatikana
Tani laki 130,000 ambazo pia tuliona zimeongezeka tofauti na miaka
iliyotangulia” Alisema Kihimbi.
Kwa
mujibu wa Bodi ya Pamba nchini Tanzania jumla ya hekari milioni 1.5 tayari zimeshalimwa pamba tofauti
na msimu uliopita ambapo ni hekari laki 6na59 elfu ndizo zilizolimwa zao hilo.
KUHUSU FURSA MBALIMBALI ZITAKAZOPATIKANA WILAYANI HUMO MARA BAADA YA ZAO HILO KUSHAMIRI NA IWAPO WAWEKEZAJI WATASIMIKA VIWANDA, FUATILIA SIMULIZI KUPITIA VIDEO HAPO JUU.
AKSANTE.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.