Kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo hatua za ubora zinavyo songeshwa na kituo Namba moja cha Redio Jembe Fm, kilicho simika makao yake Kanda ya Ziwa Victoria nchini Tanzania kunako jiji la miamba linaloitwa Mwanza.
Wakati wadau na mashabiki wake wakizidi kuongezeka siku hadi siku kupitia njia ya masafa ya kawaida yaani frequency za radio (Fm 93.7 Mwanza), nayo kasi kubwa inaendelea kushuhudiwa kwenye mtandao wa internet, Tune In, iTune na kwa Ku-Download kitufe cha Jembe Fm kupitia Google Play store, uongozi wa kituo hicho umetoa mafunzo maalum kulingana na idara zao na vitengo kwa watendaji wake kwa nia ya kuongeza chachu zaidi kwa wasikilizaji ubora.
Zaidi ya mkoa wa Mwanza, tayari Jembe Fm imepata ruksa ya kwenda mikoani na inatarajia kwenda mikoa mingine 9 kwa siku za hivi karibuni.
RATIBA ZA VIPINDI VYA JEMBE FM KWA SIKU ZA WIKI
1. MCHAKAMCHAKA SAA 06;00 - 09:00
2.SEGA LA LEO 09:00 - 11:00
3.KAZI NA NGOMA 11:00 - 13:00
4.HIT ZONE 13:00 - 16:00
5.DRIVE MIX 16:00 - 19:00
6.HOT STAGE 19:00 - 21:00
7.SPORTS RIPOTI 21:00 - 22:00
8.ASALI 22:00 - 00:00
9.PATROL 00:00 - 05:00
Japo kiduchu pata kuwasikia baadhi ya wakuu hao wa idara kupitia video hapo juu....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.