Hayo yameainishwa na Vice Counselor wa chuo hicho Tadeus Mkama, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Idadi ya wanafunzi walioshindwa kuhitimu mwaka huu imeshuka kwa asilimia 30 toka wanafunzi 750 walioshindwa mwaka jana hadi kufikia wanafunzi 424 kwa mwaka huu na hii ni kutokana na mkazo uliowekwa na chuo hicho katika kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vya juu vya uelimishaji.
Kutoka jumla ya wanafunzi 2548 ni wanafunzi 2124 ndiyo waliofuzu kukidhi vigezo vya kutunukiwa vyeti.
Asilimia 21 yaani wanafunzi 424 ndiyo walioshindwa kukidhi vigezo vya kutunukiwa ngazi mbalimbali kama vile:-
1.Astashahada.
2.Shahada.
3.Shahada 2.
4.Uzamiri.
5.Na Uzamivu.
Wanafunzi wa 4 wanategemewa kutunukiwa Shahada za Uzamivu (PHD) wawili kutoka Idara ya Mawasiliano na wa 2 kutoka Kitivo cha Sheria.
Maafali hayo ya 19 ya Chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza yanatarajiwa kufanyika siku mbili mfululizo mwishoni mwa juma hili yaani tarehe 8 na 9 ya mwezi huu Disemba 2017.
Wingi wa wahitimu wa maafali hayo umesababisha maafali kugawanywa kwa siku mbili ili kutoa fursa na wigo mpana kwa washiriki kushiriki kwa nafasi pasipo kubanwa na ratiba kuendeshwa vile inavyotakikana.
Mkama amesema kuwa chuo chake kinazingatia miiko na protokali zinazoendesha maafali na hasa ukizingatia kuwa siku hiyo ni adhimu kwa wahitimu na mashuhuda wao ambao ni familia zao.
Kabla ya maafali hayo kutakuwa na siku maalum ya Maonyesho ya Jumuiya 'Community Day' Siku ambayo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine huwaalika wadau, wanafunzi, ndugu jamaa na marafiki, makampuni na mashirika mbalimbali kwenye maonesho ya Kitaaluma ambapo wanafunzi na waadhiri hupata nafasi kuonesha masuala kadhaa wanayohusika nayo katika fani zao mbalimbali kuanzia Uhandisi, Sheria, Taaluma ya Habari, Elimu na kadhalika.
Picha ya muonekano wa jengo la utawala SAUT Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.