ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 19, 2017

HAYA NDIYO YALIYOIBULIWA NA TRL KWA UPANDE WA MWANZA.

Uongozi wa Shirika la Reli nchini TRL umefanya ziara mkoani Mwanza pamoja na kuzibaini fursa zilizopo pia kubaini kero na changamoto ambazo serikali imekusudia kuzitatua.

Kufanya maboresho na matengenezo ili kuongeza ufanisi.

Kuzungumza na wadau mbalimbali mathalani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wadau wa Marine na Bandari namna ya kuboresha upya huduma ili kuzitumia fursa zilizopo toka kwa abiria hadi usafirishaji mizigo.

CHANGAMOTO.
-Bado kuna uhaba wa mabehewa 

-Vichwa vya treni vichache tofauti na mahitaji.

-Uchakavu uliokithiri kwa njia za reli, majengo na miundombinu.

-Wafanyakazi kutopandishwa madaraja kwa muda mrefu.

-Vifaa vya kufanyia kazi kwa Mafundi wa mabehewa pindi vifaa vinapo haribika au ajali kutokea hata jeki zilizopo hazina sifa.

-Hakuna magari kwa mafundi kwaajili ya kufuatilia changamoto zinazotokea kwenye njia za treni,ajali inapotokea. Pale panapohitajika ufundi Shirika hulazimika kutuma mafundi toka vituo vya mbali kutatua changamoto ambazo zingewezwa kufanyiwa utatuzi na vituo vya karibu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.