ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 28, 2017

TGGA YAKABIDHI VYETI KWA WALIOHITIMU MAFUNZO YA MWANAMKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

 Viongozi na walimu wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakishangilia baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujitambua na ujasiri katika kambi iliyofanyika hivi karibuni  eneo la Mombasa, Dar es Salaam. Zaidi ya 36 kutoka mikoa mbalimbali walishiriki kwenye mafunzo hayo. Pia katika mafunmzo hayo yaliyofanyika kwa wiki moja yalihudhuriwa na viongozi kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar

Mgeni rasmi katika hafla ya kufungakambi hiyo yalifanywa na Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba, ambaye aliwaasa kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwenda kuanzisha kambi za kuwafundisha wanachama mikoani wanakotoka.
 Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakiruka kwa furaha
 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akimkabidhi cheti mmoja wa walimu waliohitimu mafunzo hayo.
 Grace Shaba akimkabidhi m cheti mmoja wa wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Jestina Philip
 Grace Shaba akimkabidhi cheti Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa  Lindi, Sharifa
 Grace Shaba akimkabidhi cheti Happy wa Makao Makuu ya TGGA Dar es Salaam

 Mwalimu wa Girl Guides , Valentina akikabidhiwa cheti
 Kiongozi wa Girl Guides wa TGGA, Makao Makuu, Rehema Kijazi akipokea cheti kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Grace Shsba. Katikati ni Kamishna Rose.
 Michelle kutoka Rwanda akifurahi baada ya kukabidhiwa cheti
 Kiongozi wa Girl Guides kutoka Madagascar akipokea cheti
 Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi, akipokea cheti
 Kiongozi kutoka Tanga, akipokea cheti
 Twarhiya Hussein kutoka Lindi  mtoto pekee aliyehitimu mafunzo hayo na kufanya vizuri, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba.

 Rachel Baganyila kutoka Uganda akifurahi kupokea cheti
 Ni wakati wa kucheza ngoma
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.