MAMIA ya watoto wamepoteza maisha kutokana na
homa ya uti wa mgongo nchini Nigeria, huku duru za kiafya zikiarifu
kuwa yumkini ugonjwa huo ukasambaa na kuenea katika nchi jirani ya
Niger.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na maafisa wa afya Nigeria na
kimataifa mjini Abuja imesema kuwa, watoto 336 wenye umri kati ya miaka 5
na 14 wamefariki dunia kutoka na ugonjwa huo unaojulikana kwa
Kiingereza kama 'meningitis' katika maeneo mbalimbali ya nchi.Imeogeza kuwa, kesi 2,997 za ugonjwa huo zimeripotiwa katika majimbo ya Zamfara, Katsina, Kebbi, Niger na Sokoto katika maeneo ya kaskazini magharibi na kaskazini ya kati nchini humo.
Meningitis au homa ya uti wa mgongo ni ugonjwa unaosababishwa na virusi au bakteria, ambapo tishu zinazozunguka ubongo na uti wa mgongo wa muathiriwa huungua na kudhoofika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment