MWANAMKE mmoja alifahamika kwa jina la Anastazia Francis (48,) mkazi wa kata ya Nyasaka Wilayani Ilemela amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba chake kwa kutumia mtandio.
Tukio hilo limetokea jana saa 11 asubuhi maeneo ya Nyasaka Wilayani humo ambapo marehemu alikutwa amekufa kwa kutumia mtandio aliouning’iniza kwenye dirisha juu kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza DCP.Ahmed Msangi amesema kuwa marehemu baada ya mumewe kuondoka alimtuma mwanae wa aliehitimu kidato cha nne na mwingine mdogo dukani baada ya hapo ndipo alipata fursa ya kujinyonga chumbani kwake.
Amesema tukio hilo lilijulikana baada ya mtoto wake kurudi ndani ya chumba kuchukua shati na kumkuta mama yake akiwa amejinyonga na kuanza kuiita watu ili waje kumsaidia.
“ Wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walifika eneo la tukio na kukuta mama huyo akiwa tayari amefariki dunia, lakini upelelezi unaendelea ili kufahamu chanzo cha tukio hilo na mwili wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajilo ya Uchunguzi”amesema Msangi.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkonon kwani kitendo hicho ni kosa la jinai bali pindi wanapopatwa na matatizo waombe ushauri kwa watu wengine ili kuweza kuepusha maamuzi ambayo ni hatari katika maisha yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.