Rais Yahya Jamme ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwanzoni mwa mwezi huu amesisitiza kwamba, hataachia ngazi na kuondoka madarakani.
Rkizungumza kupitia televisheni ya taifa ya Gambia hapo jana, Jammeh amesisitiza kwamba, licha ya kushindwa na mpinzani wake Adama Barrow katika uchaguzi uliopita, lakini hana mpango wa kuondoka madarakani.
Aidha kiongozi huyo amelaani vikali juhudi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS ambayo imekuwa ikijaribu kumshinikiza ili akabidhi madaraka kwa njia ya amani kabla ya kumalizika muhula wake wa uongozi Januari 18 mwakani.
Rais Jammeh amesema kama ninavyomnukuu: Mimi si mwoga. Haki yangu haiwezi kutishiwa na kukiukwa. Huu ndio msimamo wangu na hakuna mtu anayeweza kuninyima ushindi huu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu."
Awali Jammeh ambaye ameiongoza Gambia kwa miaka 22 alikubali matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi mpinzani wake, Adama Barrow na hata kumpongeza hadharani. Hata hivyo wiki moja baadaye kiongozi huyo alitengua msimamo wake huo na kutangaza kuwa kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi wa rais.
Rais mteule wa Ghana Adama Barrow akishangilia baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais. |
Awali Jammeh ambaye ameiongoza Gambia kwa miaka 22 alikubali matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi mpinzani wake, Adama Barrow na hata kumpongeza hadharani. Hata hivyo wiki moja baadaye kiongozi huyo alitengua msimamo wake huo na kutangaza kuwa kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi wa rais.
Rais Jammeh ameyakataa matokeo ya uchaguzi wa rais kwa madai ya kile alichokiita makosa yasiyokubalika yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Gambia na kutaka uitishwe uchaguzi mwingine mpya.
Msimamo huo wa Rais Jammeh umeongeza wasiwasi wa Gambia kutumbukia katika machafuko ya ndani. Hivi karibuni Rais Macky Sall wa Senegal alitangaza kuwa, kuna uwezekano rais wa Gambia kuondolewa kwa nguvu za kijeshi katika kiti cha urais baada ya kukataa kukubali kushindwa katika uchaguzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.