Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (kushoto) akiwa na mwakilishi kutoka Sahara Media Group Bi. Fatuma Shemweta. |
Naibu Wazirri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa tamashasha hilo licha ya kuwa limekuja kipindi kizuri cha sikukuu za mwisho wa mwaka bali pia limekuja na faida kuwa sehemu ya kufungua fursa kwa wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula na watoa hudua za mahoteli kutangaza na kuzitambulisha bidhaa zao kwenye jukwaa kubwa la wahudhuriaji.
"Tamasha hili tulikuwa tukilisikia tu Dar es salaam likifanyika lakini safari hii Tamasha la Vinywaji na Vyakula limegonga hodi mkoani mwetu" alisema Mama Mabula.
"Mimi nimekuja hapa tu kwa lengo moja, kwa sababu fursa tunayoipata kwanza Rock City Mall iko jimboni kwangu wilaya ya Ilemela, pamoja na kwamba itabeba wafanyabiashara wangu na wilaya ya karibu Nyamagana na Magu pia itakuza mahusiano na biashara kwa wadau wa wilaya mbalimbali zinazouzunguka mkoa ambapo wadau wake hususani watoa huduma wa mahoteli wanakutana kwa nadra sana au pengine hawajawahi kabisa kukutana" alisema na kuongeza
"Naomba kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kama sehemu ya watazamaji na wanunua bidhaa halikadhalika washiriki kama sehemu ya wadau watoa huduma na wafanyabiashara katika siku zote mbili za tukio yaani tarehe 31 mwezi Disemba 2016 kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 alfajiri ya tarehe 1 mwezi wa kwanza mwaka mpya wa 2017"
JJ Gombanila Meneja Mauzo wa Serengeti Breweries Kanda ya Ziwa |
Meza kuu Mgeni Rasmi, waandaaji na wadhamini wa Tamasha. |
Sehemu ya Wanahabari na wadau wa huduma mbalimbali za hoteli na biashara mkoa wa Mwanza. |
JJ Gombanila Meneja Mauzo wa Serengeti Breweries Kanda ya Ziwa . |
Jukwaa la habari na wapenyeza taarifa kusanyikoni. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.