Akizungumzia tukio la kuuliwa kwa Andrey Karlov aliyekuwa balozi wa Russia nchini Uturuki, Sergei Lavrov amesema kuwa, wahusika wa jinai hiyyo hawawezi kufikia malengo yao. Lavrov amesema kuwa lengo jingine la mauaji hayo ni kutaka kutoa pigo kwa uhusiano wa Moscow na Ankara na kuvuruga ushirikiano wa pande mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekumbusha kuwa, Marais wa Russia na Uturuki wamefanya mazungumzo ya simu na kukubaliana kufanya uchunguzi wa pamoja kuhusu mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki.
Balozi wa Russia akiwa ameanguka chini baada ya kupigwa risasi na mvamizi mwenye silaha. |
Balozi wa Russia mjini Ankara Andrey Karlov aliuawa jana kwa kupigwa risasi kadhaa na mtu aliyetambuliwa kuwa afisa polisi wa Uturuki. Balozi Andrey Karlov aliuawa wakati alipokuwa akihutubia maonyesho ya sanaa ya picha mjini Ankara.
Wakati huo huo Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amelaani mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki na kusema kuwa, kitendo hicho cha kigaidi ni cha kushtua.
Bi Federica Mogherini amesema Umoja wa Ulaya uko pamoja na serikali na wananchi wa Russia kufuatia kitendo kiovu cha kuuliwa balozi wa Russia mjini Ankara.
Viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Iran wametoa taarifa za kulaani mauaji hayo ya kigaidi ya balozi wa Russia nchini Uturuki na kutoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Russia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.