NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza.
KUFUATIA agizo la Waziri wa Utumishi wa Umma Angela Kairuki la usajili wa watumishi wa Umma kupitia mfumo wa usajili vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Nyamagana imenza rasmi hivi leo zoezi hilo ili kuhakikisha watumishi wanahakikiwa ikiwemo kuwatambua walio hewa.
Zoezi hilo limezinduliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mery Tesha ingawa limeanza Oktoba 3 ambapo litamalizika Oktoba 17 mwaka huu na kusema kuwa litawasaidia kuwatambuwa watumishi wanaopaswa kuwa nao na ambao ni hewa huku akiwataka kutoa ushirkiano kwa Nida.
“Zoezi hili ni lazima ili kutatua tatizo la watumishi hewa, pia zoezi litatusaidia kutambua kama bado tunawafanyakazi hewa katika Wilaya yetu”amesema Tesha.
Aidha kwenye zoezi hilo watumishi wa umma wametakiwa kuwa na vyeti vya taaluma, kitambulisho cha mpiga kura,vyeti vya Shule kikiwemo cha darasa la saba vitakavyosaidia kufanya uhakiki wa kina kwa watumishi hao.
Baada ya Mkuu huyo kutoa maelekezo hayo suala la cheti cha darasa la saba limechukua sura tofauti kwa baadhi ya walimu ambao hawana vyeti hivyo wakihofia kutopata vitambulisho vya uhakiki.
Mmoja wa walimu hao Fransic Mtunda amesema suala la cheti cha darasa la saba ni changamoto kwani baadhi ya watumishi hawajasomea katika Mkoa wa Mwanza hivyo gharama kuvifuatilia wakati muda uliotolewa ni mchache.
“Zoezi hili ni zuri, watumishi wasiusue kujisajili kwa sababu zoezi hili pia litaambatana na masuala ya uhakiki ya watumishi hewa,usipohakikiwa kupitia kitambulisho unaweza ukakatwa mshahara na ikawa changamoto nyingine kwa mtumishi” anasema Mtunda.
Kwa upande wake Afisa msajili vitambulisho vya Taifa (NIDA) Daudi Hashim amesema zoezi hili litakuwa endelelevu kwani baada ya usajili wa watumishi wa umma kumalizika zoezi hilo litahamia kwa wananchi ambapo litamalizika juni 2017.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.