ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 4, 2016

TANZANIA NA CONGO ZAWEKA SAINI MKATABA WA KUSAKA MAFUTA.

Serikali za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa kutafuta mafuta katika ziwa Tanganyika.
Mkataba huo umesainiwa ikulu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Mafuta wa DRC, Ngoyi Makena mbele ya Marais wao John Magufuli na Joseph Kabila.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Magufuli amesema ziara ya Kabila imelenga kuleta manufaa ya kiuchumi na kwamba watashirikiana kutafuta mafuta katika ziwa hilo.

Rais Magufuli amesema amekubaliana na Rais Kabila kwamba bomba la mafuta ambalo litajengwa kutoka Hoima, Uganda kwenda Tanga litatumika kusafirisha mafuta ya DRC kwenda Tanga.

"Bomba la mafuta litakuwa na manufaa mengi, sio kwa Tanzania na Uganda pekee, bali pia DRC. Tumekubaliana kwamba wakianza kuchimba mafuta watatumia bomba hilo," amesema Rais Magufuli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.