NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza.
SERIKALI imefanya mabadiliko kwenye safu ya uongozi wa tume ya maendeleo ya ushirika kwa kumteua Batholomew Haule kuwa kaimu mrajis wa tume hiyo ili kuboresha utendaji wa maendeleo ya Ushirika .
Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba amesema pamoja na kazi wanayoifanya tume hiyo, Serikali pia imedhamiria kukuza uchumi wa wananchi kwa kutumia dhana ya Ushirika.
“Serikali imefanya mabadiliko hayo na kutiliwa mkazo kufuatia hotuba ya waziri Mkuu wa alipokuwa akifungua mkutano wa nne wa bunge la kumi na mbili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo waziri kuwa watakao bainika kuhusika na ubadhirifu wa mali za ushirika kuchukuliwa hatua hivyo sitegemei makosa hayo kujirudia”, Amesema Tizeba.
Viongozi wengine waliohamishiwa moshi katika chuo kikuu cha ushirika ni Dk. Audax Rutabazimbwa ( aliyekuwa kaimu mrajisi) na Johnham Malewo (aliyekuwa kaimu naibu mrajisi) huku wengine watumishi sita waandamizi wakitakiwa kuwasili kwa katibu mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ili waweze kupangiwa vituo vya kazi.
Tizeba aliwataja Viongozi hao wapya ambao wataenda kwa katibu kupangiwa kituo cha kazi kuwa ni pamoja na Peter Kasuga, Stephenson Ngonda, Bahati Lukiko, Moshi Mukama, Marwa Nyahende, Pamoja na Juma Makili.
“Katika kuimarisha huduma za ushirika wafuatao watakaimu nafasi za warajisi wasaidizi katika mikoa ya Mtwara, Salmin Issa Lindi, Benjamini Magwala Njombe, Andrew Msafiri, na Mara ni Richard Majalla na wale waliokua wanakamu nafasi za warasijisi wasaidizi watendelea kufanya kazi kwenye vituo walivyopo sasa”, Alisema.
Hata hivyo mabadiliko hayo yamelenga katika kuboresha utendaji katika tasnia ya Ushirika huku akiwaagiza viongozi na maafisa wa ushirika kusimamia kikamilifu maendelao ya ushirika ili malengo ya kuanzisha yaweze kufikiwa ikiwa ni pamoja na kusimamia vyama utekelezaji wa sera na sheria ya ushirika
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment