WANAFUNZI IFM WATEMBELEA DUKA JIPYA LA AIRTEL EXPO
- Wanafunzi wa IT wa chuo IFM wahimizwa kushirikiana na Airtel
Wanachuo kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kitengo cha IT , wamefanya ziara ya mafunzo kwenye duka la kisasa la Airtel Expo lililopo katika ofisi kuu za Airtel mtaa wa morroco Dar es salam ikiwa ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora za kibunifu kwa wateja wake.
Wanachuo hao waliweza kujifunza mambo mengi juu ya kampuni hiyo inavyofanya kazi kuanzia huduma zake hadi bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo. Ikiwemo Modem iliyozinduliwa hivi karibuni maarufu kama modem ya maajabu Wingle Modem inayouweza kutumika na zaidi ya watu 10 kwa wakati mmoja, Simu za Kisasa za gharama nafuu na zenye OFA nzuri
Wanafunzi hao pia wamejionea jinsi duka la Airtel Expo linavyohudumia wateja wengi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kidigitali.
Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba amewapongeza wanafunzi hao kwa dhamira yao ya kutaka kujifunza katika ulimwengu wa technolojia na kuwakaribisha wengine kuhudhuria'
tumefarijika sana kuona wanafunzi toka vyuo vya ndani ya nchi yetu kama nyie IFM mnafunga safari na kuja kushuhudia hili, hongereni sana tunawakaribisha wote sio tu wanafunzi bali kila mpenda maendeleo ya technolojia kutembelea duka hili la kisasa na kujionea au kushauriana na Airtel kufanya mambo mengi bora zaidi ya ulimwengu wa mawasiliano" alisema Bi Lyamba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.