ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 29, 2016

BAADA YA UCHAGUZI KUMALIZIKA, HUU NDIYO MSIMAMO WA TFF KUHUSU RAIS MPYA WA FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) lilitoa tamko kabla ya uchaguzi wa rais wa FIFA kwamba, Afrika pamoja na vyama vyake vya soka vitamuunga mkono Sheikh Salman katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika February 26, 2016.


Mbali na CAF kutoa agizo kwa vyama vyake vya soka kumuunga mkono Sheikh Salman bado mgombea huyo alishindwa kufurukuta mbele ya Gianni Infantino ambaye alishinda kiti hicho cha urais kwa tofauti kubwa ya kura na kuashiria huenda kuna nchi wanachama wa CAF hawakumpigia kura Sheikh Salmani.

Shaffihdauda.co.tz imefanya mahojiano maalumu na rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi kutaka kujua hasa ni kitu gani kimemuangusha Sheikh Salman licha ya Afrika bara lenye kura nyingi kutangaza kumuunga mkono rais huyo wa shirikisho la soka la Asia.

“Tumepata rais mpya wa FIFA sasa Gianni Infantino nimeongea na waandishi wa habari wa kimataifa na sasa naongea na Clouds TV, Clouds FM na shaffihdauda.co.tz ni kwamba tumekubali matokeo ya uchaguzi, uchaguzi ni uchaguzi kikubwa sasahivi ni kutoa ushirikiano kwa rais mpya Infantino na kuhakikisha mpira duniani unaendelea na tunaamini kwa dhati kabisa sasa tumeondoka kwenye hali ya mtikisiko tuliyokuwanayo baada ya matatizo yaliyotokea chini ya mzee Blatter Katibu Mkuu wake pamoja na Michel Platini na wengine”.

“Yalitokea matatizo lakini sasa ule mtikisiko umekwisha sasahivi mpira Afrika umetulia, Asia umetulia, America umetulia, Ulaya umetulia  kwahiyo sasa tutulie tutengeneze mpira wetu na tunaamini kwa dhati kabisa kama shirikisho la mpira wa miguu Tanzania tumepata kiongozi Gianni Infantino na tunaamini tutasonga mbele”.

Shaffihdauda.co.tz: Infatino amekuwa rais wa FIFA, sera zake zinaiangalia Afrika na Tanzania kwa ujumla au kwasababu amekuwa rais inabidi twende nae hivyohivyo?

Malinzi: Rais wetu Gianni Infantino aliongea mambo mengi sana kwenye manifesto kwa maana ya ilani. Ukisoma ilani yake imezungumzia mambo makubwa sana siyo kwa ajili ya Afrika lakini kwa ajili ya mpira wa dunia lakini kikubwa kuliko vyote ni kwamba, rais wetu Infantino sasa ni muda wake wa kubadilisha mpira wa Afrika, Asia, Oceania, Amerika Kusini na Kati na Ulaya na dunia kwa ujumla.

Ndiyo muda sasa wa kutuunganisha ili mpira uweze kuonekana ukichezwa kwa umoja kwa maana ya dunia.

Shaffihdauda.co.tz: Kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza, watu wengi walikuwa wanampa nafasi Sheikh Salman hasa baada ya bara la Afrika kuonekana kum-support ambalo ndiyo block lenye kura nyingi pamoja na bara lake la Asia, lakini Sheikh Salman tangu mwanzo kabisa alipata kura chache dhidi ya infatino. Nini kimetokea kwa mtazamo wako?

Malinzi: Shirikisho la soka barani Afrika walitoa tamko kwa maana kamati ya utendaji ya CAF kwamba wanam-support Sheikh Salman, lakini tamko ni tamko na wapiga kura ni wapiga kura. Wapiga kura wameamua kufanya walichokifanya na niseme tu kwamba uchaguzi umekwisha kilichobaki tucheze mpira.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.