ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 4, 2015

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA HAKUNA AFISA MSAIDIZI TUNAYEMSHIKILIA KWA KASORO ZA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25 MWAKA HUU

Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Mwanza ambao waliwakilisha vyombo vyao kuripoti masuala ya uchagzuzi.
NA PETER FABIAN, MWANZA.
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limeleleza kwamba hakuna Afisa msaidizi yoyote wa Tume ya Uchaguzi linayemshikilia kutokana na kasoro za uchaguzi zilizojitokeza wakati wa kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo katikika majimbo yote tisa yaliyopo Wilaya saba za mkoani hapa.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo,  nameweka bayana jana alipozungumza na waandishi wa habari Ofsini kwake, alikanusha kwa kueleza kwamba taarifa zinazodaiwa kutolewa na kuenezwa Wilayani Ukerewe kwamba Maafisa wasaidizi watatu wa Tume ya Uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya hiyo walikamatwa na Jeshi la Polisi kutokana na kukutwa na mabosi ya kura.
 
Mkumbo alisema kwamba taarifa hizo siyo za kweli na hakuna Afisa anayeshikiliwa na Polisi na kufafanua kwamba kilichojitokeza Wilayani humo baada ya kutangazwa matokeo ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Nduligu akiwa na Kaimu Mweka Hazina, Baraka Mnuo na Kaimu Afisa Utumishi aliyemtaja kwa jina moja la Mussa, kufatilia masaduku ambayo hayakuwasilishwa siku hiyo Ofisi za Halmashauri.
 
“Baada ya Nduligu, Mnuo na Mussa kuonekana na masanduku hayo kulijenga hofu kwa wafuasi na viongozi wa Chama kimoja cha siasa na kuanza kuwashutumu kuwa pengine walifanya ujanja wa kutoa matokeo kwa kuongeza kura vituoni, taarifa hizi zilifika Kituo cha Polisi Wilaya na kilichofanyika watumishi hao walihojiwa tu kisha wakaachiwa kuendelea na majukumu yao baada ya kuonekana hakukuathili matokeo hayo.
 
Kamanda aliongeza kuwa baada ya kuhojiwa walitoa maelezo yao ambapo waliwajulisha viongozi wote wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ikiwemo mawakala na wagombea ili kuondoa malalamiko na walikubaliana na kuamua kuyafuata lakini badae baadhi ya watu wakaanza kusambaza taarifa kuwa walikamatwa na masanduku ya kura jambo ambalo siyo kweli.

 
Mkumbo alisema kwamba katika Mkoa wake huo hakuna uvunjifu wa amani uliotokea siku ya uchaguzi isipokuwa kutokana na kasoro za zoezi la upigaji kura katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mwanza na Manspaa ya Ilemela kujitokeza kutokana na changamoto hiyo baadhi ya watu kupata mihemuko na kutaka kufanya vurugu lakini ulinzi uliokuwa umeimarishwa walikamatwa.


“Watu hao hawakuvuruga zoezi la upigaji kura wala utangazwaji wa matokeo hivyo polisi waliwadhibiti na kuwakamata kabla ya kuleta madhara na kesho yake walifikishwa Mahakamani na wanaendelea na mashauri yao waliyofunguliwa (bila kutaja idadi ya waliokamatwa na kuwafikisha Mahakamani) lakini mambo yalikwenda vizuri na Mkoa uko  shwari,”alisema.
 
Kamanda Mkumbo aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa upigaji kura hadi kutangazwa matokeo kwa utulivu na amani uliokuwepo kwenye vituo vya kuhesabia na kutangazia matokeo, hadi sasa wananchi wa maeneo mbalimbali wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi na maendeleo ikiwa ni wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi na wafugaji bila hofu yoyote.
 
Wito wangu kwa wananchi tuendelee kuvumiliana hasa kwa wale wenye mihemuko na ushabiki wa kisiasa kwa kuwa uchaguzi umeishapita na tujikite kushirikiana katika shughuli za maendeleo na tuwakatae watu wachache wasiotutakia mema kwa kutuhamasisha katika uchochezi wa kuivuruga amani jambo ambalo tukiwakubalia tutaanza vurugu na amani iliyopo itatoweka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.