NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wametakiwa kuachana na vitendo vya anasa na kufanya uhuni na badala yake wahakikishe wanaepukana na tabia hiyo ili wasije kukatisha masomo yao kutokana na kutapa mimba za utotoni pamoja na kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo wakati wa sherehe za mahafali ya kumi ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Kibaha independent iliyopo Wilayani Kibaha.
Ndikilo amesema kwamba wanafunzi wanapaswa kuacha na mambo ambayo hayana faida kwao na badala yake wahakikishe wanasoma kwa bidii zote ili kuweza kuliletea maendeleo Taifa la Tanzania katika siku za mbeleni na sio kushiriki katika katika masuala ambayo hayana manufaa yoyote.
Alisema kwamba ana imani endapo Taifa likiwa na wasomi wengine katika kila kona kutaweza kuleta chachu kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi hivyo kunatakiwa kufanyike juhudi za makusudi kuwalinda wanafunzi na kuhakikisha wananapatiwa elimu katika mazingira ambayo ni rafiki kwao ili waweze kufaulu kwa kiwango cha juu.
“Jamani kitu kikubwa ambachi ninataka kukisema hapa sio kwa wanafunzi mnaomalizi leoo hii katika shule ya independent bali ujumbe huu ni kwa wanafunzi wa Tanzania nzima kuacha na tabia ya kuendekeza anasa na kufanya uhuni hii mimi kwa kweli siipendi hata kidogo hivyo inatakiwa kuachana nayo mara moja na kitu cha msingi ni kuongeza juhudi katika masomo yenu,”
“Wakati mwingine wanafunzi wanajikuta wanasahau kabisa majukumu yao ya kusoma kwa bidii, kwa hivyo mimi nina imani kuwa wakiachana na mambo hayo wataweza kufika ambali kwani wakati mwingine tumeshuhudia wanafunzi wanakatisha masomo yao kutokana na kupata mimba wakati wapo shuleni hasa kwa upande wa wasichana hii ni hatari sana,”alisema Ndikilo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawafuatilia watoto wao kwa ukaribu ili kuweza kjua maendeleo yao katika masomo pindi wanapotoka shuleni kwa kuwakagua madaftari na mambo mengine ambayo yanahusiana na elimu ili kuweza kutambua changamoto zinazowakabili.
Katika hatua nyinge Ndikilo aliseza kutumia fursa ya kuwaasa walimu wasikubali kutishwa na mtu yoyote katika kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na nafasi ya urais unaotarajiwa kufanyioa octoba 25 mwaka huu na badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila kuwa ya kuwa na uwoga wowote kwani ulinzi upo wa kutosha.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa shule hiyo ya Kibaha Independent Hezron Musalale alisema kuwa malengo ya shule hiyo ni kuhakikisha wanafunzi wote pindi wanapomaliza shule wanajua kusoma na kuandika kwa ufasaha katika lugha ya kingereza pamoja na Kiswahili lengo ikiwa ni kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wakurugenzi wa shule hiyo Yusufu Mfinanga alisema kwamba shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2002 ina malengo ya kuongeza kasi ya ufaulu kwa anafunzi wake kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Pwani pamoja na wazazi na walezi ili kuinua ubora wa elimu na ustawi wa ukuaji wa kiuchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.