ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 8, 2015

MKUU WA MKOA WA PWANI AWATAKA VIJANA WALIOMALIZA MAFUNZOYA JKT KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

NA VICTOR MASANGU, PWANI   DATE 8 RC NA JKT

MKUU wa Mkoa wa Pwani  Injinia Evarist Ndikilo amewataka vijana hapa nchini waliomaliza mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) kuhakikisha hawatendi mambo ambayo yapo  kinyume na maadaili na badala yake  wawe wazalendo  wa dhati katika kuilinda nchi yao katika mipaka yote  ya ndani na nje ili iwe ya utulivu na  amani. 

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameitoa wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya JKT yanayojulikana kama Operesheni Kikwete kwenye kambi ya Ruvu iliyopo Mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mhandisi Ndikilo amebainisha kuwa endapo  vijana hao waliomaliza mafunzo hayo wakiwa na umoja, kuijari na kuitetea nchi ya Tanzania kwa hali na mali ya  uwajibikaji na bila  ya kuwa na ubaguzi wowote ule kutaweza kuleta mabadiliko chanya kupitia mafunzo waliyoyapata katika kujenga Taifa imara.

CUE IN ..1 RC NDIKILO

Kwa upande wake Brigadia Jenerali Jacob Kingu ambaye alimwakilisha mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga amesema kuwa kwa sasa  kuna vijana waliopata mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa JKT wapatao  67,239  kuanzia machi 2013 hadi kufikia mwaka 2015 ikiwa inafahamika kama  operesheni Kikwete.
 CUE IN 2..MEJA MUHUNGA
Hata hivyo brigadia JENERALI Kingu amesema kwa sasa kuna makambi 12 ambayo yanatoa mafunzo hayo lakini hayakidhi mahitaji hivyo kushindwa kuwachukua wanafunzi wote wanaohitimu kidato cha sita wanaopaswa kujiunga .

Nae  Mkuu wa kikosi cha 832 Ruvu JKT Luteni Kanali Charles Mbuge amebainisha kuwa katika mafunzo hayo  vijana wamejifunza mambo mbali mbali ikiwemo matumizi ya siraha,matumizi ya ramani, uraia,usalama na utambuzi vitu ambavyo ni mkombozi mkubwa na vyenye tija katika Taifa la Tanzania.

CUE IN..KANALI MBUNGE
 
Hata hivyo Luteni Kanali Mbunge amesema
 kikosi hicho bado kinakabiliwa chanagamoto ya ukosefu wa X-ray hali ambayo inawalazimu kuwapeleka wagonjwa katika hospitali teule ya rufaa ya Tumbi na wakati mwingine kuwapeleka hospitali ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam  ambako kuna umbali mrefu.

Mafunzo ya  jeshi la  kujenga Taifa JKT kwa vijana hao  yalianza rasmi mnamo machi 2013 yakiwa na idadi ya vijana 15110 na kufikia idadi ya vijana 19993 kwa mwaka huu wa 2015 sawa na asilimia 15.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.