ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 7, 2013

YANGA YALALA 2-1 DHIDI YA KCC

Ziara ya Mabingwa katika mchezo wa pili wa marudiano baina ya Yanga na KCC ya Uganda uliochezwa leo jioni dimba la CCM Kambarage umeshuhudia Mabingwa Yanga wakila kichapo cha bao 2-1.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Lufunga (kulia) akiwa na kombe la Ubingwa la soka Tanzania bara lililoletwa na mabingwa wa msimu wa 2012-2013 Yanga African ambao walicheza mchezo wa kirafiki wa marudiano na KCC katika Uwanja wa CCM Kambarage na Yanga kuchapwa 2-1. 

Kabla ya mchezo huu wa marudiano kocha wa KCC aliwatahadhalisha Yanga kuwa makini wawapo mchezoni, lakini hii leo Yanga wamerudia makosa yale yale kwa safu yake ya ulinzi kukosa umakini na kujisahau mara kadhaa nao KCC kutumia makosa hayo kujipatia ushindi.

Mchezaji wa KCC Kyambabe Allan akijaribu kutafuta nafasi  kutoa pasi kwa wachezaju wenzake wakati huo huo wachezaji wa Yanga wakijipanga kuunasa mpira, katika mchezo wa pili wa marudiano wa kirafiki uliochezwa katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga. 

Brother wa Mwanza naye ndani ya dimba la CCM Kambarage Shinyanga..

Wadau wakiwa na kamanda mpiganaji (kulia)

Wadau wa blogu hii (G. Sengo) mjini Shinyanga.

Engo na vyombo vya usafiri.

Mashabiki.

Faulo...

Jamaaa naye alitia timu Shy Town.

Matokeo hayo hayakuwa na madhara yoyote kwa mashabiki wa Yanga mkoani Shinyanga, wakijua kabisa ni sehemu ya mazoezi kwa timu yao nao waliendelea kufanya maandamano uwanjani kwa kuzunguka na kombe la ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara walilolitwaa msimu wa 2012-2013.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.