Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi (kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda 1-0. |
Mchezaji Kelvin Matale wa Mwanza (kushoto) akichuana na Dickson Mwesa wa of Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda 1-0. |
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Levi Nyakundi akikabidhi mfano wa hundi kwa mchezaji bora wa Airtel Rising Stars Anna Hebron kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
Timu ya Mwanza ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za Airtel Rising Stars kwa mwaka 2013 |
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam |
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam |
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za fainali |
Mwanza mabingwa ARS 2013
· Kinondoni wasichana watwaa kombe
Timu ya Mwanza wavulana imeibuka kidedea katika michuano ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga Morogoro 1-0 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Nayo timu ya Kinondoni wametwaa taji la wasichana kwa kuifunga Ilala 1-0.
Goli pekee la Mwanza lilifungwa na mshambuliaji machachari Athanas Mdam kwa shuti kali katika dakika ya 34. Mdam amejizolea sifa kem kem baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli na kutangazwa kuwa mfungani bora wa fainali hizo.
Mbali na Mdam, wachezaji wengine waliong’aa katika mashindano hayo na kuchaguliwa na jopo la makocha ni Arafat Mussa (mlinda mlango bora) kutoka Kinondoni na Omary Hussein (mchezaji bora) kutoka Ilala.
Vile vile wachezaji sita (wasichana watatu na wavulana watatu) wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye kliniki ya kimataifa ya soka kwa vijana itakayofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na kusimamiwa na makocha kutoka shule za mafunzo ya soka za Manchester United. Wachezaji hao ni Anna Hebron, Niwael Halfan, Shelda Boniface, Athanas Mdam, Thomas Chindeka na Omary Hassan.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetaja majina ya timu za wavulana na wasichana yakayofanyiwa mchujo ili kupata wachezaji 16 kutoka kila upande kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria mwezi Septamba.
Wachezaji hao kwa upende wa wavulana ni Arafat Mussa, Fred Bakari, Emmanuel Innocent na Willy Karolo (Kinondoni), Aziz Hassan, Omary Hussein, Joseph Mushi, Saddy Said na Said Danda (Ilala), Rothan Mkanwa, Petro Mgaya, George Chota, Ramadhani Kondo na Optamus Lupekenya (Morogoro), Bruno Shayo, Luseke Kiggi, Martini Lusseke na Athanas Mdam (Mwanza), Thomas Chindeka, Miraji Kingaye na Salum Issa (Temeke) na Michael Bosco (Mbeya).
Wasichana ni Najihati Abbas, Stumai Abdallah, Anastazia Anthon, Tatu Iddi, Shelda Boniphace, Rehema Yahya na Anna Bebron (Kinondoni), Niwael Halfan, Amina Ramadhan, Latifa Ahmed na Alafa Abdul (Temeke), Vumilia Maharifa, Donisia Daniel, Maimuna Khamis na Amina Ally Ilala), Khadija Hiza (Tanga), Mwamvita Tabago, Shakila Hashimu na Zainabu Bakari (Kigoma), Shamimu Ally na Farida Mohamed (Ruvuma).
Akiongea wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa kliniki na mashindano ya Nigeria yatawapa fursa zaidi ya kujifunza na kupata uzoefu na kusisitiza nia ya kampuni ya Airtel kuendeleza kudhamini mashindano hayo.
Naye mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo Amos Makala aliwataka vijana kuonyesha vipaji vyao na kuyataka makapuni mengine kujitokeza kudhamini michezo. Wito wake uliungwa mkono wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Leodegar Tenga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.