ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 16, 2013

MWINYI KAZIMOTO AINGIA MITINI WAKATI TAIFA STARS IKIINGIA KAMBINI MWANZA KUJIANDAA NA MCHEZO WA MARUDIANO NA UGANDA

Taifa stars wako jijini Mwanza eneo ambalo si mara ya kwanza kulitumia kama sehemu ya kambi ya mazoezi.

Katika mazoezi ya leo Kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na benchi lake la ufundi walionekana wako bize wakivigawa vikosi mafungu kwa mafungu bila shaka ilikuwa ni mbinu ya maboresho kwa kila idara kulingana na mikakati iliyowekwa.
Canavaro akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake timu ya Taifa huku kocha mkuu wa timu hiyo Poulsen na msaidizi wake Marsh wakitizana kwa makini kinachoendelea.

Poulsen akitoa maelekezo kwa Chuji (mwenye bips ya blue) kwenye mazoezi hayo yanayofanyika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Wakati mazoezi hayo yakiendelea Shirikisho la soka nchini TFF limekiri taarifa za kutoweka kambini bila taarifa kwa mchezaji kiungo wa Timu ya Taifa Stars Mwinyi Kazimoto, ikiwa ni mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita.
Afisa habari wa TFF Richard Wambura amethibitisha taarifa za kutoweka kwa mchezaji huyo... SIKILIZA kwa kubofya play..
Kocha Kim Poulsen akitoa maelekezo kwa vitendo kwa wachezaji wa timu yake.

Kutoka kushoto ni mmoja kati ya makocha benchi la ufundi Taifa Stars, Afisa Habari wa TFF Michael Wambura na mdau wa soka Mwanza Mr. Kayombo wakiangalia mazoezi ya Stars yaliyofanyika katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza jioni ya leo. 

Pumzi zaidi.

'Run'

Wito umetolewa kwa mashabiki wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla kumiminika kwa wingi Kampala nchini Uganda siku ya mchezo ili kutoa sapoti yaushangiliaji kwa Taifa Stars kwenye mchezo wa marudiano.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.