Radio call (simu ya upepo) iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza marehemu Liberatus Barlow hatimaye imenaswa ikiwa imefichwa kwenye shimo la maji taka (septic tank) kwenye moja ya nyumba eneo la Nyashana jijini Mwanza.
Kunaswa kwa Radio call hiyo kumekuja kufuatia kukamatwa kwa watu wengine watatu zaidi wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.
Watu hao waliokamatwa mara baada ya kutajwa na washirika wenzao watano ambao tayari wako mahabusu ni pamoja na Abdalah Petro Ndayi (32) mkazi wa Mjimwema jijini Mwanza, Abdalahman Ismail (28) mkazi wa Mkudi Ghana, na Lyoba Matiku anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 46-50 akiwa ni mkazi wa Nyakabungo jijini Mwanza huyu anatajwa kuwa ndiye mfadhili wa kundi hilo la ujambazi na mipango yote ya uvamizi hufanyika kwake.
Msikilize kwa kubofya play Mkuu
wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya Jinai wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo anafafanua zaidi...
Vielelezo
vingine vilivyokamatwa nyumbani kwa mtuhumiwa Abdalah Petro Ndayi ni pamoja na
Ufunguo mmoja wa gari alilokuwa akiendesha Kamanda Liberatus Barlow siku ya
tukio, sim card za mitandao mbalimbali, simu nne za mkononi kila moja ikiwa na
laini yake, kofia mbili aina ya barreti kati ya hizo moja ni ya polisi na
nyingine ni ya kampuni ya ulinzi.
Vielelezo
vingine ni sare moja (suruali na shati) ya rangi ya blue yenye mstari mweupe ya
moja ya makampuni ya ulinzi jijini Mwanza, suruali moja ya kaki
inayofanana na sare za mgambo wa jiji la Mwanza ikiwa na masalia ya damu kwenye
pindo la suruali kwa nyuma, kipande cha nondo, bisibisi na sare inayotumiwa na
askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU...
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.