ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 5, 2012

SIMBA VETERANI YAISHINDA YANGA VETERANI PENATI 4-2 UWANJA WA MAGOMENI KIRUMBA

Timu ya Veterani wa Simba Kata ya Kirumba wakiwa katika picha ya pamoja.

Timu ya Veterani wa Yanga Kata ya Kirumba wakiwa katika picha ya pamoja.
Niwakati wa fair play...

Mgeni rasmi wa mchezo baina ya maveterani wa Simba na Yanga kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mwanza, Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza (Nyamagana) Stanslaus Mabula (kulia) akifatilia mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Magomeni Kirumba pembeni yake ni Bw. Peter Mashashi mdau wa soka kata ya Mkolani.

Sehemu ya ummati wa mashabiki uliofurika katika uwanja wa Magomeni kushuhudia mechi hiyo ya msisimko...

Nahodha wa timu ya Yanga Veterani Khamis Ommary akikabidhiwa kikombe kidogo cha mshindi wa pili na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula.

Nahodha wa timu ya Simba Veterani Jackson Robert aka 'Jack Fish' akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, baada ya kuibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya watani zao Yanga Veterani.

Jack Fish pia ni mwasisi wa mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kudumisha mahusiano, kuboresha afya na kujikumbusha ujuzi wa kusakata kabumbu enzi hizo za ujana. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.