Akithibitisha taarifa hizi Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Bugando Dr. Charles Majinge amesema kuwa "Ni kweli Mhashamu Baba Askofu Balina amefariki majira ya saa tano asubuhi ya leo na alikuwa amelazwa hospitalini hapa akitibiwa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kansa"
Marehemu Mhashamu Baba Askofu kabla ya kuwa askofu wa jimbo katoliki Shinyanga alikuwa Askofu wa kwanza wa jimbo Katoliki la Geita kabla ya kuhamishiwa jimbo kuu la Shinyanga.
Taratibu za mazishi na taarifa zaidi zitatolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hivyo waumini wanataarifiwa kuwa watulivu kwa kipindi hiki na kumwombea marehemu wakati tukisubiri kutangazwa rasmi.
Bishop Aloysius A. Balina alizaliwa june 21st 1945 katika mji wa Isoso, Ntuzu wilayani Bariadi; na kupewa daraja la U-Askofu tarehe 06 January 1985
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Tupe maoni yako
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
ReplyDeleteRaha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie. apumzike kwa amani. Amina.
ReplyDeleteMungu ailaze mahali pema Mhashamu Askofu Balina. AMINA
ReplyDelete