BENDI Kongwe ya mziki wa dansi nchini Tanzania Msondo Music inatarajia kuzindua vyombo vyake vipya kabisa walivyokabidhiwa hivi karibuni na Kampuni ya KONYAGI akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema tumeshapewa vyombo na Konyagi ambavyo tutavizindua mbele ya mashabiki wetu siku ya Ijumaa pale LIDAZ CLUB siku ya Ijumaa hivyo wapenzi wote wa bendi ya Msondo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili kuona vyombo vipya
Pamoja na kupata burudani za bendi hiyo zikiwemo nyimbo za zamani na za sasa kwa ajili ya kuanza wik end Super D aliongeza kwa kusema wapenzi watakaokuja siku hiyo watapata burudani za radha tofauti tofauti kwani wamepanga kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kutumia vyombo vyao vipya
Bendi hiyo siku ya Jumapili itamaliza burudani za wik end katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni
Mkurugenzi wa Bendi hiyo Muhidini Maalimu Gulumo ataongoza kundi zima la wana msondo ngoma akiwemo Said Mabera, Shabani Dede, Romani Mn'gande, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hassani Moshi na wendine kibao kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.