ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 20, 2018

WAZIRI WA MAJI ATANGAZA KUSITISHA TENDA KWA MKANDARASI HUYU WILAYANI BUNDA


GSENGOtV
Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa ametangaza Wizara ya Maji  kutompa zabuni ya mradi wowote Mkandarasi wa kampuni ya Nyakirang'anyi  inayotekeleza mradi wa maji wa Bunda Mjini ambao una zaidi miaka miwili haujakamilika.

Mbarawa ameyasema hayo mara baada ya kukagua kazi ya utandazaji wa bomba  kuu la  maji inayofanywa na Mkandarasi huyo, chanzo cha maji Nyabehu na mradi wa maji kijiji cha Kinyambwiga.

Kampuni ya nyakirang'anyi inatekeleza kwa gharama ya bilioni 1.7.

Waziri akikagua baadhi ya miradi ya maji..
Usimikaji wa mabomba ukiendelea wilayani Bunda.

Thamani ya mradi wa kwanza ambao umenuia kutoa maji toka kwenye busta hadi kwenye tank ni Bilioni 1.75 na urefu wake ni km 4.3.

KAZI za mradi ni kutandaza bomba toka kwenye busta iliyopo kijiji cha Migunganyi kupeleka kwenye tanki lililopo mlima Kaswaka. 2016, mradi uliopashwa kukamilika tangu 2017 mwanzoni, ambapo hadi sasa haujakamilika,

Pia kulaza mabomba yenye upana wa mililita 300 umbali 4.3, kujenga chemba 3 na kulaza pira 24.....  44 Bl2.4 lakini awali ilikuwa km 32 (2014-16)  

Sasa mkandarasi huyo amepewa muda kufikia 29 mwezi huu (Novemba 2018) kukamilisha vioski 16 na kufunga mita za maji 1000 za wateja kwaajili ya majaribio ya awali na ukaguzi.
Waziri Mbarawa akitoa maelekezo ya pumpu ya maji.
Injinia Maisha akionesha miundombinu ya maji.
Miundo mbinu....Waziri Mbarawa akioneshwa miundombinu ya maji.
Chanzo cha maji.
Sehemu ya mji wa Bunda uliokosa maji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.