Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NINAYO, Jack Langworthy akiwa ameshika tuzo aliyopewa kwenye maonyesho ya Wajasiriamali ya AMBA 2018 yaliyofanyika jijini London hivi karibuni.
LONDON: Kampuni ya Kitanzania ya NINAYO, imeshinda Tuzo ya Ubora ya MBA (MBA Excellence Awards) katika maonyesho ya kijasiriamali. Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, Jack Langworthy wa NINAYO, ameipokea tuzo hiyo ya mwaka wakati wa chakula cha jioni tuzo zilizoandaliwa na Chama cha AMBAs (AMBA) tarehe2 Februari 2018 jijini London.
NINAYO.com ni mtandao wa biashara wa kilimo uliotumiwa na wakulima zaidi ya 30,000 na masoko katika Nyanda za juu Kusini ya Tanzania ambapo ilifanya tukio la kukumbukwa Ijumaa usiku. Lengo la kuanzisha tovuti ni kwamba: Kuwapa wakuliama na soko taarifa wanazohitaji kuunganisha kwa ufanisi zaidi.
NINAYO inatoa huduma hIyo bure, kwa wale wanaotumia mitandao ya Airtel na Vodacom kwa kuingia kupitia tovuti ya 0.freebasics.com/ inayokuunganisha moja kwa moja kwenye mtandao.
Alipoulizwa kuhusu huduma hiyo, Langworthy alielezea, "Bei ya bidhaa daima itakuwa ni ile unayoweza kufanya makubaliano. Niliona wakulima wengi wakiwa na uwezo mdogo wa kufanya makubaliano wakati kipindi tunajitolea kupitia Peace Corps. Volunteer. Kulikuwa na fursa ya kuwawezesha wakulima kwenye kupata habari za biashara ambazo zingewasaidia kuwainua kutokana na umaskini. Kupitia NINAYO sasa wakulima wanaweza kuwasiliana na mamia ya wanunuzi moja kwa moja, kwa njia ya simu, SMS, au kwenye tovuti. Wanunuzi wanapenda pia tovuti pia na kila mtu anafanikiwa."
NINANYO ilizinduliwa Tanzania mwaka 2015 na inatumia vyanzo vingi vya data ili kutoa mwanga wa biashara kwa watumiaji wake. Watumiai wa NINAYO zaidi ni wakulima wadogowadogo ambapo wanaweza kupata pesa nyingi kwa kuuza maradufu kupitia mfumo huo wa biashara. Kwa kuondokana na madalali, wakulima na masoko wanaweza kufanikiwa.”
NINAYO imeanza kutumia data za kibiashara zilizokusanywa kwa kutoa mikopo ya majaribio kwa wakulima wasiojiunga na benki kwa ushirikiano na UNCDF DF+
NINAYO imeleta uwekezaji kutoka kwa Silicon Valley na kuwekeza nchini Tanzania kupitia washirika wao Expa Labs ambako huko wajasiriamali wengi wamefanikiwa.
NINAYO alipata hamasa zaidi na kuweka mkazo kutoka kwa San Francisco inayoendeshwa na mwanzilishi mwenza wa Uber, Garrett Camp, ambazo teknolojia zao zinatikisa kwenye ulimwengu wa teknolojia kimataifa.
" Tanzania imekuwa ikionekana kama nchi maskini. lakini Tanzania ni nchi yenye fursa nzuri. Kuna mamilioni ya Watanzania wenye vipaji wanaotaka kujenga ustawi wa nchi yao. Shukrani kwa Expa Labs, tunaunganisha Silicon Valley na Bonde la Ufa na kubadilisha taswira ya kilimo cha Kiafrika. "
NINAYO pia iliidhinishwa katika hotuba ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama wakati wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wajasiriamali (GES) uliofanyika Silicon Valley tarehe 25 Juni 2016.
Jack Langworthy aliongeza: “Tuzo hii iliyotolewa kwa kampuni Kitanzajnia inaonyesha uwezo wake katika ukanda wa Afrika Mashariki. Sisi hatujitolei au NGO, lakini kampuni inawekeza Tanzania kwa sababu tunaamini ni nchi nzuri yenye vipaji. Nairobi ni sehemu nzuri lakini haikutazanwa, kwa sababu Dar es Salaam inakuwa kitovu kipya cha teknolojia. "
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.